02 – Mtiririko/ Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake
Makala namba 02:
السجود الصحيح (2
2 – Sijida sahihi
قال رسول الله – صلى الله عليه وسلم-:
Amesema Mtume – Swala na Salamu za Allah ziwe juu yake:
” أُمِرْتُ أنْ أسْجُدَ علَى سَبْعَةِ؛ أعْظُمٍ علَى الجَبْهَةِ، وأَشَارَ بيَدِهِ علَى أنْفِهِ واليَدَيْنِ والرُّكْبَتَيْنِ، وأَطْرَافِ القَدَمَيْنِ ”
Nimeamrishwa kusujudu juu ya viungo saba; juu ya paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake juu ya pua yake, na mikono miwili na magoti mawili na ncha za nyayo mbili.
رواه البخاري (٨١٢)
Maelezo:
Mzazi /Mlezi mfundishe mtoto wako: Mwanangu kusujudu ni nguzo katika nguzo za swala na katika nguzo hii kunadhihiri unyenyekevu na mja kujidhalilisha kwa Mola wake – aliyetukuka – pale ambapo anaweka paji lake la uso juu ya ardhi na uso ni kiungo kitukufu zaidi katika mwili. Na hapa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – anatufundisha namna ya kusujudu yaani ni wajibu hivi viungo saba visujudu navyo ni:
1 – Paji la uso pamoja na pua (1)
2 – Mikono miwili (2)
3 – Magoti mawili (2)
4 – Na ncha za vidole vya miguu miwili /nyayo) (2)
Jumla viungo saba (7).
Mtiririko huu ni wenye kuendelea Allah akitaka, Usikose namba tatu [3].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️
Imechapishwa: February 17, 2021M, Rajab 5, 1442H.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•