01 – Sifa za mume ambaye anatakiwa mwanamke amchague kwa ajili yake

https://t.me/fawaidussalafiyatz

صفات الزوج الذي ينبغي أن تختاره المرأة لنفسها.

SIFA ZA MUME AMBAYE ANATAKIWA MWANAMKE AMCHAGUE KWA AJILI YAKE

Makala namba 01:

من هذه الصفات ما يلي:

Miongoni mwa hizi sifa ni (hizi) zifuatazo:

١ – أن يكون ذا دين وخلق لقوله تعالى: { وَلَعَبْدٌ مُؤْمِنٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ } البقرة ٢٢١ ولقوله – صلى الله عليه وسلم – (إِذَا خَطَبَ إِلَيْكُمْ مَنْ تَرْضَوْنَ دِينَهُ وَخُلُقَهُ فَزَوِّجُوهُ إِلَّا تَفْعَلُوا تَكُنْ فِتْنَةٌ فِي الأَرْضِ وَفَسَادٌ عَرِيضٌ) روى الترمذي (١٠٨٤) وابن ماجة (١٩٦٧) وحسنه الألباني في صحيح الترمذي.

1 – Awe ni mwenye dini na tabia njema kwa kauli yake (Allah) aliyetukuka: { Na mtumwa mwanaume muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni }

Al-baqarah: 221

Na kwa kauli yake (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie: { Atakapotaka kuoa kwenu yule ambaye mnairidhia dini yake na tabia yake basi muozesheni, kama hamkufanya hivyo (hamkumuozesha) kutakuwa na fitna ulimwenguni na ufisadi mwingi }.

Ameipokea Tirmidhiy na Ibn Majah.

Maelezo:

Hii ni sifa ya kwanza ambayo mwanamke /wasimamizi wa mwanamke wanatakiwa waitizame pindi anapokuja mtu kumchumbia binti yao au Dada yao n.k, iangaliwe dini yake je, itikadi yake ni sahihi, ameshika suna sawa sawa na kufuata mwenendo wa wema waliopita, je anaswali swala tano na mengine yanayowajibika juu yake. Wakiridhizika naye basi wamuozeshe na wala wasiangalie mali wakaacha kumuozesha kwa sababu kufanya hivyo ndiyo sababu ya kutokea mabalaa ya uzinifu kwa kubakia mabinti wengi bila ya kuolewa na vijana wa kiume kutooa Kisha waichunguze tabia yake wasimuozeshe mwanaume mwenye tabia mbaya, au mpumbavu wanatakiwa wajue kuwa ndoa ni safari ndefu na ndoa ni msingi wa kujenga familia na familia ndiyo sehemu ya jamii kwa hiyo kutengemaa kwa jamii ni lazima kupatikane familia zilizoshika dini sawa sawa.

itaendelea Allah akitaka, usikose makala ijayo …

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 13, 1442H ≈ February 25, 2021M,

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz Darsa za ndoa Jiunge hapa: ⤵️ https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *