04 – Mtiririko/ Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah swala na salamu za Allah ziwe juu yake Makala namba 04:
قَالَ رَسُوْلُ اللَّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلّمَ
Amesema Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:
أكثرُ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ الْجَنَّةَ تَقْوَى اللّٰهِ وحُسْنُ الخُلُقِ
Kitu ambacho (mara) nyingi mno kitawaingiza watu peponi ni kumcha Allah na tabia njema.
رواه الترمذي ( ٢٠٠٤)
Maelezo:
Mzazi /Mlezi mwambie mwanao kuwa: Katika maneno, vitendo na hali ambazo humuweka mtu karibu na Allah na humfanya ni katika watu wa peponi ni kumcha Allah, na kumcha Allah: Ni kumuogopa na kumchunga kwa kujiepusha na yale aliyoyakataza na kuyafanya yale aliyoyaamrisha, Na jambo la pili ambalo litawaingiza watu wengi peponi ni tabia njema, kwa maana mtu awe na tabia njema asimuudhi yeyote kwa kauli au kitendo na wala hatamki isipokuwa yale yanayomridhisha Allah – aliyeshinda na kutukuka – Maana ya hadithi hii ni: Sababu ambayo itawaingiza peponi watu kwa wingi ni kumcha Allah na tabia njema.
Mtiririko huu ni wenye kuendelea Allah akitaka, Usikose namba tano [5].
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 14, 1442H ≈ February 26, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•