03 – Sifa za mume ambaye anatakiwa mwanamke amchague kwa ajili yake

صفات الزوج الذي ينبغي أن تختاره المرأة لنفسها.

SIFA ZA MUME AMBAYE ANATAKIWA MWANAMKE AMCHAGUE KWA AJILI YAKE

Makala namba 03:

٣ – أن يكون مستطيعا للباءة بنوعيها فإن النبي صلى الله عليه وسلم – حث الشباب على الزواج عند استطاعتهم الباءة.

3 – Awe ni mwenye uwezo wa tendo la ndoa /gharama za ndoa kwa sababu Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – amewahimiza vijana juu ya ndoa pindi watakapokuwa na uwezo wa kimwili /gharama za ndoa.

أي: القدرة على الجماع والقدرة على مؤن النكاح وتكاليفه وتكاليف المعيشة.

Maana yake: Uwezo wa tendo la ndoa na uwezo wa gharama za ndoa na ya lazima katika hiyo (ndoa) na ya lazima katika maisha.

وقد قال النبي- صلى الله عليه وسلم – لفاطمة بنت قيس: أما معاوية فصعلوك لا مال له.

Na bila shaka Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie alimwambia – Fatuma bint Qais: Ama Muawiyah ni Fakiri hana mali.

Faida na maelezo: Na wala hadithi hii haipingani na kauli yake Allah – aliyetukuka:

{ وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ ۗ .. }

{ Na waozesheni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Kama watakuwa ni mafakiri Allah atawatosheleza kwa fadhila zake ..} نور ٣٢

Hakuna shaka kuwa dini akipingana na chochote hutangulizwa dini lakini hapa tunakusudia pindi watakapolingana watu wawili waliokuja kuposa wote wakawa wamesimama sawa sawa katika dini, lakini mmoja wao ni mwenye uwezo na wa pili ni masikini hohe hahe bila shaka huyu mwenye uwezo atatangulizwa kama vile Mtume – swala na salamu zimfikie – alivyompa ushauri Fatumah bint Qais – Allah amridhie – Kisa chake kwa ufupi ni hiki kama kilivyokuja katika sahihi Muslim: Anasema Fatumah bint Qais – Allah amridhie: Kuwa mumewe alimuacha talaka tatu (mara tatu) na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – hakumpa haki ya kukaa kwa huyo mume (aliyemuacha) na wala haki ya chakula, ila Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – aliniambia: Pindi utakapomaliza eda nifahamishe, basi (alivyomaliza eda) wakamchumbia watu watatu: Muawiyah, na Abuu Jahm, na Usamah bin Zaid, basi akasema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie: Ama Muawiyah ni mtu hohe hahe hana mali, ama Abuu Jahm ni mtu mwenye kupiga mno wanawake lakini olewa na Usamah bin Zaid, basi (Fatuma) akafanya mkono wake hivi (kwa kuchukia): Usamah! Usamah! basi Mtume wa Allah akamwambia: Kumtii Allah na kumtii Mtume wake ni bora kwako ” akasema (Fatuma): Basi nikaolewa naye, basi nikaonewa choyo (kwa heri nyingi niliyopata).

رواه مسلم ١٤٨٠

Maelezo: Maana ya hadithi hii kuwa: Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alimtajia ufakiri wa huyu mchumba kwa kuchunga haja ya wanawake ya kuhitajia mali kwa sababu anahitajia kula, kuvishwa na mengineyo.

قال شيخ الإسلام ابن تيمية في “مجموع الفتاوى ( ٢٨/٢٣٠) : “فَبَيَّنَ لَهَا أَنَّ هَذَا فَقِيرٌ قَدْ يَعْجِزُ عَنْ حَقِّك”

Amesema Sheikh l-islam ibn Taimiyyah – katika Maj-mu’ul-fatawaa (28/230): “Basi (Mtume) akambainishia huyo (mwanamke) kuwa huyu ni fakiri huwenda akashindwa kutekeleza haki yako

” وقال الشيخ ابن عثيمن- رحمه الله – في “لقاءات الباب المفتوح” (١٤/٢٣١) الشاملة .

Na amesema Sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu- katika liqaatul-baabi l-maftuuh (14/231)

“وهذا دليل على أن للمرأة أن ترد الخاطب إذا كان فقيراً، ولكن الأفضل إذا كان ذا خلق ودين أن تتزوج به ” .

” Na hii ni dalili kuwa mwanamke anaruhusiwa kumkataa mchumba akiwa fakiri lakini ni bora zaidi akiwa ni mwenye dini na tabia njema aolewe naye ” Ufafanuzi: Haina maana kuwa mwanamke amkatae mwanaume mwenye dini na tabia njema na aolewe na mwanaume asiyeshika dini kwa sababu ya wasaa wa mali alio nao! bali kama watagongana wote wakawa na dini si vibaya akamchagua huyo mwenye wasaa wa mali, lakini dini ni lazima. itaendelea Allah akitaka, usikose makala ijayo …

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab16, 1442H, Feb 28, 2021M.

1 Comment

  1. Mussa kikoko

    Maashaallah nimefaidika kwa kiasi kikubwa,. Alhamdulillah

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *