Mfululizo wa makala kuhusiana na masuala ya biashara; Makala ya pili [2]

https://www.fawaidusalafiya.net

MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA!

MAKALA NAMBA 02;

MASUALA MUHIMU:

الفرق بين بيع السلم وبيع ما ليس عندك.

Tofauti baina ya biashara ya kutanguliza thamani na kuchelewesha bidhaa na biashara ya kuuza kile usichokuwa nacho:

1 – Biashara ya salam si kuuza kile anachokimiliki mtu mwingine, bali biashara ya salam ni kuuza kitu ambacho kinakuwa katika shingo yako yaani muuzaji anajibebesha majukumu ya kukileta kwa muda mtakaokubaliana na kile kitu kinakuwa hakipo kwa muda ule kwa maana kama gari itatengenezwa baadae, au mazao yatalimwa baadae, kwa sharti maalumu ambazo zinatajwa katika vitabu vya fiqih.

2 – Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa hii biashara ya salam ni maalumu kwa bidhaa zinazopimwa kwa mizani na ujazo.

3 – Biashara ya salam ni lazima thamani itolewe yote katika kile kikao ambacho mnunuaji na muuzaji wanauziana.

Mwisho:

Kwa kifupi kuna tofauti baina ya biashara ya kutanguliza thamani na bidhaa kuletwa baadae ambayo inaitwa “Salam” ambayo muuzaji anakielezea kitu ambacho atakikabidhi kwa mnunuzi kwa baadae na kitu chenyewe hakipo kwa muda ule kwa maana kinakuwa ni deni kwa muuzaji, mfano: ukamkabidhi pesa mkulima wa mpunga kwa makubaliano ya kukupa mpunga baada ya kuvuna, muamala huu unaruhusiwa kwa sharti maalumu zilizoelezwa katika vitabu vya fiqihi. Ama kuuza kitu ambacho mtu hana kwa maana hakimiliki ni kama hii biashara inayofanywa na baadhi ya watu ambayo mtu anachukua pesa ya mtu na kumuuzia bidhaa fulani hali ya kuwa bidhaa hana yaani ipo kwa mtu mwingine na yeye hajaimiliki bado, biashara hii ni haramu. Allah akitaka tutaandaa makala inayofuata tutaelezea biashara ya “Salam” yaani biashara ya kutanguliza thamani ya kitu na kuchelewesha bidhaa, ambayo ina masharti kadhaa pindi yatapokamilika basi biashara hiyo itakuwa ni halali na haya tuliyoyataja hapa ni baadhi tu, ili watu wapate kujua tofauti baina ya biashara hiyo na biashara hii iliyoharamishwa ya kuuza kile usichokimiliki.

ITAENDELEA.. Usikose makala namba 03 in shaa Allah.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net. Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 21, 1442H ≈ March 5, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Abubakar Mutayoba

    ،،،
    Ni mada nzuri sanaاَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *