https://t.me/fawaidussalafiyatz
صفات الزوج الذي ينبغي أن تختاره المرأة لنفسها.
SIFA ZA MUME AMBAYE ANATAKIWA MWANAMKE AMCHAGUE KWA AJILI YAKE
Makala namba 04:
٤ – يستحب أن يكون رفيقا بالنساء، وذلك لأن النبي – صلى الله عليه وسلم – قال في شأن أبي جهم:
4 – Inapendeza awe mpole kwa wanawake na hilo ni kwa sababu Mtume – swala na salamu zimfikie – alisema katika jambo la Abuu Jahm:
أمَّا أبو جَهْمٍ فلا يَضعُ عصاهُ عن عاتقِهِ .. انكِحي أسامةَ بنَ زيدٍ .. ”
Ama Abuu Jahm haitoi fimbo yake mabegani mwake …olewa na Usamah bin Zaid ..
Maelezo:
Katika sifa za mume mwema anatakiwa awe mpole kwa mkewe /wakeze. Ndiyo Mtume – swala na salamu zimfikie – alimtahadharisha Fatumah bint Qais – Allah amridhie – kuolewa na huyu Abuu Jahm kwa sababu alikuwa hana huruma na wanawake alikuwa mpigaji sana kwa wanawake. Na hii ndiyo kawaida ya Mtume wetu – swala na salamu za Allah zimfikie – yaani huruma na upole kwa wanawake, kama anavyosimulia Anas bin Malik – Allah amridhie –
– كانَ النبيُّ صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ في مَسِيرٍ له، فَحَدَا الحَادِي، فَقالَ النبيُّ صَلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ: ارْفُقْ يا أنْجَشَةُ، ويْحَكَ بالقَوَارِيرِ.
(Siku moja) Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alikuwa katika safari yake basi akawa (mmoja wao) anawapeleka ngamia kwa haraka na hali ya kuwa akiimba mashairi, basi akasema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie: Kuwa na huruma ewe Anjashah, tahadhari na chupa. البخاري Ufafanuzi: Huyu Anjashah alikuwa akiupeleka huu msafara kwa haraka na ndani yake kulikuwa na wake zake Mtume – swala na salamu zimfikie – na kwa huruma aliyokuwa nayo Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alimuamrisha apunguze mwendo na akawafananisha wanawake na chupa kwa udhaifu wao na unyonge, wapo kama ilivyokuwa chupa isipotunzwa inaweza kuvunjika kwa haraka na hivi ndivyo walivyo wanawake wanahitajia huruma, upole.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 22, 1442H ≈ March 6, 2021M,
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz Darsa za ndoa Jiunge hapa: ⤵️ https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•