Mfululizo wa makala kuhusiana na masuala ya biashara; Makala ya tatu [3]

https://t.me/fawaidussalafiyatz

MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA!

MAKALA NAMBA 03;

HUKUMU ZA BIASHARA YA KUTANGULIZA THAMANI NA KUCHUKUA BIDHAA BAADAE.

Maana ya biashara hii:

Kuuza kitu kitakachotolewa baadae kwa thamani inayotolewa sasa hivi. Mfano ukaenda kwa mkulima wa mpunga ukamtaka akuuzie mpunga kilo kadhaa, lakini kwa sasa mpunga hana yaani haupo bali atakuja kulima na kuvuna kwa hiyo mnunuzi atatoa thamani yote ya huo mpunga katika kikao cha kuuziana na wala haifai kulipa nusu au kubakisha sehemu ya malipo na sharti nyinge tutazieleza katika makala inayofuata ambazo zikikamilika basi biashara hii itakuwa sahihi. Na biashara hii imeitwa “salam” kwa sababu thamani yake hicho kinachonunuliwa ni lazima yote itolewe katika kikao cha kuuziana. Biashara hii imethibiti kwa qurani na hadithi sahihi na makubaliano ya wanachuoni, Ama katika Qurani ni kauli yake Allah – aliyetukuka:

﴿ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنْتُمْ بِدَيْنٍ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ﴾

{ Enyi mlioamini pindi mnapokopeshana deni (fulani) kwa muda ulio tajwa (uliowekwa), basi andikeni }.

البقرة: ٢٨٢ قال ابن عباس: أشهد أن السَّلَف المضمون إلى أجل مسمى قد أحله الله في كتابه وأذِن فيه، ثم قرأ هذه الآية.

Amsema ibn ‘Abbas – Allah amridhie: Nashuhudia kuwa biashara ya kutanguliza thamani iliyodhaminiwa kwa muda maalumu bila shaka Allah ameihalalisha katika kitabu chake na ameiruhusu kisha (ibn Abbas) akaisoma aya hii (tuliyoitaja). Na katika suna amepokea ibn Abbas – Allah amridhie – amesema:

أن رسول الله – صلى الله عليه وسلم- قدِم المدينة وهم يُسلِفون في الثِّمار السنة والسنتين والثلاث، فقال: (مَن أسلف في شيءٍ، فليُسلِف في كيل معلوم، ووزن معلوم، إلى أجل معلوم)

Kuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alifika katika (mji wa) Madinah hali ya kuwa hao (watu wa Madinah) wananunua matunda kwa kutanguliza thamani, (na bidhaa inatolewa baada) ya mwaka au miaka miwili au mitatu, basi akasema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- :

” Mwenye kununua /kuuza kwa kutanguliza thamani katika chochote basi auze /anunue kwa kutanguliza thamani katika ujazo maalumu na uzito maalumu kwa muda maalumu.

أخرجه الستة.

Ufafanuzi wa hadithi hii:

Maana ya hadithi hii ni kuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie alipohamia Madinah aliwakuta watu wa Madinah wakiuza na kununua kwa aina hii ya biashara ya kutanguliza thamani inayotolewa katika kikao cha kuuziana na kuchelewesha bidhaa, Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – aliwawekea sharti maalumu. Kama vile uzito /ujazo maalumu, muda maalumu na sharti nyingine ambazo wanachuoni wamezichanganua tutazitaja katika makala inayofuata ambayo tutazungumzia sharti tu. Dalili ya tatu ya kufaa kwa biashara hii ni: Makubaliano ya wanachuoni: Wamekubaliana wanachuoni kuwa aina hii ya biashara ni halali kwa sababu watu wana haja ya aina hii ya muamala kwa sababu wakulima, wafanya biashara wanahaja na muamala huu wa kutoa thamani na kuchelewesha bidhaa, kwa sababu wao huwa na mahitaji ya nafsi zao au kuhudumia mashamba yao, sheria akaruhusu muamla huu kwa kuwaondolea tabu na shida.

ITAENDELEA.. Usikose makala nammba 04 in shaa Allah.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net.

Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Rajab 25, 1442H ≈ March 9, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *