https://t.me/fawaidussalafiyatz
MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA!
MAKALA NAMBA 04;
SHARTI ZA BIASHARA YA KUTANGULIZA THAMANI NA KUCHUKUA BIDHAA BAADAE.
يشترط لصحة السلم سبعة شروط؛ وهي:
Kunashurutishwa ili iwe sahihi biashara ya kutanguliza thamani na kuchelewesha bidhaa (salam) sharti saba nazo ni:
أحدها: أن يكون فيما يمكن ضبط صفته.
1 – (Sharti ya) ya kwanza yake: Iwe katika ile (bidhaa) inayowezekana kudhibitiwa sifa zake.
فتاوى اللجنة الدائمة – المجموعة الأولى . باب السلم (١٤/٩٣)
Ufafanuzi wa mfasiri: Ni lazima aina hii ya biashara ya kutanguliza thamani na kuchelewesha bidhaa inatakiwa iwe bidhaa ambayo inadhibitika ima kwa kilo (uzito) au ujazo, au urefu au idadi mfano: Nafaka, matunda, unga, pamba, chuma, dawa, mayai, n.k . Ama zikiwa bidhaa ni katika zile ambazo hazidhibitika kwa sifa hizi haziruhusiwa kuuzwa kwa namna hii bali ni lazima ziuzwe hali ya kuwa zipo mfano kama: Nyumba, viwanja, ngozi za wanyama, mbao, vitu hivi na mfano wa hivi hata ukibainisha jinsi yake na aina yake na sifa yake na kiwango chake ni lazima kuna hali ya kutofahamika kwa kiasi kikubwa itakuwepo hali ambayo inapelekea mizozo mfano: Kuna tofauti kubwa baina ya ngozi ya mnyama huyu na ngozi ya mnyama mwingine, baina ya lulu hii na lulu hii. Kwa kifupi: Zinatakiwa sifa za hiyo bidhaa zijulikane na ni ya aina gani, mfano: Maharage ya mbea, au gari aina fulani ina sifa hizi na hizi .n k.
ITAENDELEA.. Usikose makala namba 05 itakayoelezea sharti ya pili in shaa Allah.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net.
Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Sha’aban 01, 1442H ≈ March 14, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•