https://t.me/fawaidussalafiyatz MFULULIZO WA MAKALA ZINAZOHUSIANA NA MASUALA YA BIASHARA!
MAKALA NAMBA 05;
SHARTI ZA BIASHARA YA KUTANGULIZA THAMANI NA KUCHUKUA BIDHAA BAADAE.
الثاني: أن يصفه بما يختلف به الثمن ظاهرا.
2 – (Sharti ya) pili: (Muuzaji) aielezee sifa zake kwa (sifa) ambazo zinatofautisha thamani (ya aina ya bidhaa hiyo) kidhahiri.
فتاوى اللجنة الدائمة – المجموعة الأولى . باب السلم (١٤/٩٣)
Maelezo:
Anatakiwa muuzaji aelezee sifa ya hiyo bidhaa sifa ambazo zinatofautisha thamani yake kama vile abainishe jinsi ya hiyo bidhaa kama vile: Pamba, au mpunga, ngano, gari n.k, na pia abainishe aina yake mfano pamba ya aina gani na mpunga wa aina gani, ngano ya aina gani kama umelimwa kwa kilimo cha kumwagilia au umenyeshewa na mvua tu, na kama hiyo bidhaa ina daraja mbali mbali kwa ubora kutokana na kuzidiana ubora basi abainishe daraja lake na kiwango cha uzuri wake. Makusudio ya sharti hii ya pili ni kuwa muuzaji aeleze sifa ya hiyo bidhaa kwa maelezo ambayo yanapinga kutokea udanganyifu na kutofahamu kutokea mizozo.
ITAENDELEA.. Usikose makala namba 06 itakayoelezea sharti ya pili in shaa Allah.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net. Tembelea website yetu: ☟ https://www.fawaidusalafiya.net Telegram bonyeza hapa: ☟ https://t.me/fawaidussalafiyatz 🗓️ Imechapishwa: Sha’aban 04, 1442H ≈ March 17, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾 https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•