Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE .
Makala namba (3)
{ وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ ٱلْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعْقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَٰقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ } ( ٦ )
Na mfano wa hivyo (ulivyojiona ktk ndoto) Mola wako mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya ndoto.Na atatimiza neema zake juu yako (kwa utume na ufalme) na juu ya ukoo wa Yaa’qub , kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq.Hakika Mola wako Mlezi ni Mjuzi mwenye hekima .
سورة يوسف ١٤
Maelezo :
Baba yake Nabii Yusuf -amani iwe juu yake- akamfasiria mwanaye hiyo ndoto kuwa yeye Yusuf atateuliwa na Allah -aliyetukuka- kwa kupewa utume na atapewa elimu ya hadithi za vitabu vya Allah ,na elimu ya kufasiri ndoto na hii pia ni neema kwa ukoo wa Yaqub -amani imfikie- kama alivyowatimizia neema hiyo kwa baba zake Ibrahim na Is-haq -amani iwe juu yao- na hawa ni mababu zake lakini Allah amewaita kuwa ni baba zake hii ni dalili kuwa babu anaitwa baba na ndio maana katika madhehebu ya wanachuoni wengi zaidi babu anawazuia ndugu katika mirathi kwa sababu yeye yupo katika daraja la baba .
Na pale Allah aliposema :
{Hakika Mola wako Mlezi ni mjuzi mwenye hekima} .
Maana yake : Allah ni mjuzi anamjua yule anayestahiki kupewa neema hii ,na Mwenye hekima humpa neema hii anayemtaka kwa hekima anayoijua .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 16, 1442H ≈ April 28, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•