Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE- 04 .
Makala namba (4) :
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka :
{ لَقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ } ( ٧ )
{ Bila shaka katika (kisa) cha Yusuf na ndugu zake kuna mazingatio mengi Kwa wanaouliza }
Maelezo :
Kisa cha nabii Yusuf -amani iwe juu yake- na ndugu zake kina mazingatio makubwa ,na mawaidha ,na maajabu ndani yake ,mfano wa yale yaliyopo katika kisa hiki ni :
Husuda za ndugu wa Yusuf kwa Yusuf na mwisho wa hiyo husuda ,na jinsi Allah alivyoithibitisha ndoto ya Yusuf -Amani iwe juu yake- ,na jinsi Yusuf alivyosubiri juu ya matamanio , na juu ya utumwa na juu ya kufungwa gerezani ,na baada ya yote haya baadae akapewa utawala .Pia tunajifunza kuwa husuda haizuii lile ambalo Allah amelikadiria ,
na pia ndani yake tunaona uvumilivu wa Yaqub /baba wa Yusuf -Amani iwe juu yake- pale alipo potelewa na wanawe .
Na mazingatio mengine mengi wanayoyataja wanachuoni katika kisa hiki .
ITAENDELEA ..
Usikose tarjama ya aya ya 8 ,inshaa Allah .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 17, 1442H ≈ April 29, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈•