MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF-AMANI IWE JUU YAKE-

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF – AMANI IWE JUU YAKE –

Makala namba (5):

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

إِذْ قَالُواْ لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَى أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلالٍ مُّبِينٍ

  1. (Kumbuka) pindi (ndugu wa Yusuf) waliposema : “Bila shaka Yusuf na ndugu yake wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi na hali ya kuwa sisi ni kundi (kubwa). Hakika baba yetu yupo katika kosa lililo wazi}

Maelezo :

Ndugu zake Yusuf – amani imfikie – kwa baba walisema kuwa: Yusuf na ndugu yake ambao baba mmoja na mama mmoja wanapendwa sana na baba yetu kuliko wao .Na hali ya kuwa wao ni wengi na wenye kumsaidia zaidi baba yao, na wakaona kuwa baba yao yupo katika makosa ya wazi katika kumpenda kwake Yusuf na nduguye .

Hapa tunaona kuwa ndugu zake Yusuf hawakukanusha kuwa wao hawapendwi bali wameona kuwa Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi ,na hawakujua kuwa mapenzi huyaweka Allah katika moyo wa amtakaye huwenda huyu ukampenda zaidi kuliko huyu ,ndio maana Allah – aliyetukuka – akasema kuhusu wanawake -:

وَلَن تَسْتَطِيعُوٓاْ أَن تَعْدِلُواْ بَيْنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُواْ كُلَّ ٱلْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلْمُعَلَّقَة.

Na hamutoweza kufanya uadilifu baina yake (katika mapenzi ya moyo), japokuwa mtapupia (hilo), kwa hiyo msiegemee (upande mmoja) kabisa kabisa, mkamuacha (huyo mwingine akawa) kama aliyetundikwa .

النساء ١٢٨.

Kwa hiyo mtu hawezi kuyaondoa mapenzi ya moyo kama alivyokuwa Yaqub kwa Yusuf na mwanaye mwingine, kinachokatazwa ni kuelekea upande mmoja kwa vitendo ama mapenzi ya moyo hili halipo katika miliki ya mwanadamu.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 18, 1442H ≈ April 30, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *