MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE-

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MAZINGATIO KATIKA
KISA CHA NABII YUSUF -AMANI IWE JUU YAKE-

Makala namba (11) :

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَّبْكُوْنَ (١٦)

Wakaja kwa baba yao usiku hali wakilia .

قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِنْدَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنْتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ (١٧)

Wakasema : “Ewe baba yetu !Hakika tulikwenda kushindana mbio /kutupa mishale na tukamuacha Yusuf penye mizigo yetu ,basi mbwa mwitu akamla ; lakini wewe hutatuamini ingawa tunasema kweli “

Maelezo:

Ndugu wa Yusuf baada ya kumuweka ndugu yao ndani ya kisima wakachelewa kurudi kwa nyumbani kwao mpaka usiku ilipoingia na walifanya hivi ili wakatoe hoja kwa baba yao kuwa walimtafuta muda mrefu ! na pamoja na mbinu hii waliyotumia wakaongezea mbinu ya kulia kwa muda mrefu kwa kujifanya kumuhuzunikia Yusuf , ndiyo maana hapo Allah ametumia kitendo cha muda wa sasa kinachoonesha kuwa waliendelea kulia muda mrefu ,na hapa tunajifunza kuwa unapokuwa unasikiliza kesi au unapoletewa mashtaka usihadaike na kilio cha mwenye kuleta madai ya kudhulumiwa mpaka alete ushahidi wa wazi kama alivyosema ibn Kathir – Allah amrahamu- katika tafsir ya aya hii :

‏”ولهذا قال بَعْضُ السَّلَفِ : لَا يَغُرَّنَّكَ بُكَاءُ الْمُتَظَلِّمِ؛ فرُبَّ ظَالمٍ وَهُوَ بَاكٍ!”.

“Kwa ajili hii wamesema baadhi ya wema waliopita:

” Kisikuhadae kilio cha mwenye kudai kuwa amedhulumiwa na huwenda dhalimu (akawa) ni mwenye kulia”.

Basi ndugu wa Yusuf wakadai kuwa wao walienda kushindana kutupa mishale au kukimbia na wakamuacha Yusuf katika mizigo yao ili awe hapo na awalindie mizigo yao na akaliwa mbwa mwitu na wakamwambia baba yao kuwa hatowaamini juu ya haya waliyoyazungumza kuhusu Yusuf na hilo ni kwa sababu baba yao alikuwa akilichelea hili juu yao , au huwenda baba yao hajawaamini kwa sababu ya kutokuwa na ushahidi wa kweli juu ya maneno yao .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 13, 1442H ≈ May 25, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *