12- Mtiririko /Mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah zimfikie-
Makala namba 12:
إِكْرَامُ الضَّيْف:
Kumkirimu mgeni:
قال – صلى الله عليه وسلم-:
مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللَّٰهِ واليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ،
Amesema – swala na salamu za Allah ziwe juu yake -:
{ Yeyote aliyekuwa anamuamini Allah na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake }
متفق عليه.
Maelezo:
Katika uzuri wa dini yetu ya kiislamu na katika adabu ya dini yetu ni kumfanyia wema mgeni,
Na wajibu wa kumhudumia mgeni ni siku tatu, siku ya kwanza yaani mchana wake na usiku hii ndiyo siku ya kumkirimu vinono na mwenyeji ajilazimishe kufanya hivyo hata kama anajogoo lake kubwa basi alichinje ama siku zilizobakia atamlisha chakula chake cha kawaida yaani anachokula yeye mwenyewe.
Na tabia ya kukirimu wageni ni tabia ambayo Waarabu walikuwa nayo kabla ya uislamu na walikuwa wakishindana na kujifaharisha kwa hilo,
Kama anavyosema mshairi akielezea kawaida ya waarabu kipindi hicho:
ضربوا بمدرجة الطريق قبابهم …
يتقارعون على قرى الضيفان
Wameweka mahema yao njiani…
Wakishindana juu ya kuwalisha (kuwakirimu) wageni.
Mtiririko huu ni wenye kuendelea Allah akitaka , usikose makala namba 13, in Shaa Allah..
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 15/ Shawwal, 1442H ≈ 27/ May, 2021M.
Tembelea website yetu:
https://www.fawaidusalafiya.net
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
JIUNGE NASI TELEGRAM KUPATA FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA.
BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•