Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
أثر عجيب
ATHARI (HABARI) YA AJABU
ذكر الحافظ ابن حجر رحمه الله أن ابن عبدالبر رحمه الله أخرج بسند جيد عن أبي داود صاحب السنن : « أنه كان في سفينة فسمع عاطساً على الشط حمد الله، فاكترى قارباً بدرهم حتى جاء إلى العاطس فشَمَّته ثم رجع.
Ametaja Hafidh bin Hajar -Allah amrahamu-kwamba ibn Abdil-Barr-Allah amrahamu- ameitaja (habari) kwa sanad mzuri kutoka kwa Abuu Dawuud mwenye (kitabu cha) sunani :
kuwa yeye (Abuu Dawuud) alikuwa katika jahazi ghafla akamsikia (mtu) mwenye kupiga chafya ufukweni (na) akamshukuru Allah ,basi (Abuu Dawuud) akakodi mtumbwi kwa dirhamu (moja) mpaka akaja kwa (huyu) aliyepiga chafya akamuombea dua ( yakumrahamu) ,kisha akarudi (katika jahazi) .
فسُئل عن ذلك فقال : لعلّه يكون مجاب الدعوة، فلما رقدوا سمعوا قائلاً يقول : يا أهل السفينة ؛ إن أبا داود اشترى الجنة من الله بدرهم »
basi akaulizwa kuhusu hilo ,akasema : Huwenda (yule mtu) akawa ni mwenye kujibiwa dua ,basi pindi walipolala walimsikia (kwenye ndoto)mwenye kusema akisema :
Enyi watu wa jahazi :Hakika Abuu Dawuud amenunua pepo kutoka kwa Allah kwa dirhamu (moja) ”
[ فتح الباري ( ٦٢٦ / ١٠ )
Maelezo ya mfasiri:
Hivi ndivyo walivyokuwa watu wema waliopita ,walikuwa na pupa ya kufufua mwenendo wa Mtume -swala na salamu za Allah zumfikie- na walikuwa na pupa ya kudhihirisha kheri ili watu wapate kuwaiga katika kheri .
Hebu fikiria : Mtu anakodi mtumbwi utakaompeleka ufukweni ili akamuombee dua yule aliyepiga chafya na kumshukuru Allah !lakini leo hii sisi tunatoa ya kununua nyembe ya kunyoa ndevu zetu ,yaani tunatoa pesa kwa ajili ya kuondoa mwenendo wa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ,na hapa ndipo utapojua kuwa kwanini wenzetu walikuwa na utukufu katika huu ulimwengu mpaka makafiri wakawa chini yao ,na sisi tupo katika hali hii ya udhalili na unyonge !! tunamuomba Allah atuongoze katika haki na atudumishe mpaka kifo .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 19, 1442H ≈ May 31, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•