HUKUMU YA KUSOMA ELIMU ZA KIDUNIA .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

HUKUMU YA KUSOMA ELIMU ZA KIDUNIA .

السؤال (٥٢٣)
Swali (523)

سئل العلامة الفوزان -حفظه الله-

Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-fauzani- Allah amuhifadhi-

ما رأي فضيلتكم فيمن يتعلم من المسلمين الطب والمخترعات الحديثة بقصد إغناء المسلمين عن الحاجة إلى الكفار والمشركين‏؟‏

Ipi rai (yenu enyi) wabora katika wale waislamu wanaojifundisha tiba na (mambo) yanayovumbuliwa sasa (kama kutengeneza silaha,n.k ), kwa makusudio ya kuwatosheleza waislamu wasiwahitajie makafiri na washirikina ?

الجواب

Jawabu :

لا بأس في ذلك، ويؤجر عليه، لكن بشرط أن يكون قد تعلم من دينه ما يحتاج إليه؛ فلابد أن يتعلم أولاً أمور الدين الضرورية التي لا يعذر أحد بتركها،

Hakuna ubaya katika hilo,na analipwa (thawabu) juu ya hilo lakini kwa sharti awe amejifundisha yale anayoyahitajia katika dini yake ,basi hakuna budi kwanza ajifundishe mambo ya lazima ya dini ambayo hapewi udhuru yeyote kwa kuyaacha ,

ثم يتعلم بعد ذلك أمور الطب وغيرها من العلوم، أما أن يقبل على أمور الطب والعلوم الأخرى؛ وهو يجهل أمر دينه؛ فهذا لا يجوز‏.‏

kisha atajifundisha baada ya hapo mambo ya tiba na mengineyo katika elimu ,ama akaelekea (kusoma) mambo ya tiba na elimu nyingine ,na hali ya kuwa yeye hajui mambo ya dini yake ,hali halifai .

المنتقى فتاوى الشيخ الفوزان

Maelezo ya muandaaji:

Haifai muislamu kujishughulisha na kusoma elimu ya dunia na hali yakuwa hajui mambo ya wajibu katika dini yake ,kujifundisha yale ambayo usipojifundisha anapata dhambi kama vile na la mwanzo kabisa ni kujifundisha elimu ya tauhidi /kumpwekesha Allah ajifundishe tauhidi na ayajue yale yenye kuvunja tauhidi yake , Swala,Funga ya Ramadhani, akiwa na mali ni lazima ajifundishe somo la zaka, akitaka kuoa au kuolewa ajifundishe mambo ya ndoa ,akifanya biashara ajifundishe masuala ya biashara n.k.

Na hapa nawausia wazazi ambao wanawapeleka watoto wao mashuleni tena wengine wamebaleghe na hali ya kuwa hawajui chochote katika dini yao ,unaweza ukamuona mtoto wa kike amebaleghe na wala hajui chochote kuhusu damu ya hedhi ,nifasi,istihihadha, na wala hajui hijabu !, hawa wazazi watakuja kuulizwa siku ya kiama juu ya watoto hawa .

Kwa kifupi kila jambo linalowajibika kulitenda katika dini au unalotakiwa kulitenda ni wajibu ujifundishe ili ulifahamu usije ukaingia katika madhambi .

Hakuna katazo la kusoma elimu ya dunia ikiwa mtu amejifundisha yale yanayimuajibikia katika dini yake ,bali akisoma elimu ya dunia na akaweka nia ya kuwasaidia waislamu kwa huo ujuzi anaousomea Allah atamlipa kwa nia yake .

Ama ukawa ni daktari bingwa wa kinywa na hali ya kuwa kinywa chako hakiwezi hata kutamka suratul-fatiha ,au ukawa mhandisi hodari mwenye kujenga majumba makubwa ya kupendeza lakini haujui ibada mbalimbali za kuijenga akhera yako ! ,haujui hata kutawadha !ukiwa hivi tambua kuwa hii ni hasara na baada ya kujua hili ,tenga muda ujifundishe mambo ya wajibu katika dini yake .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 27, 1442H ≈ Jun7, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *