https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
HII NDIYO TIBA YA MARADHI HAYA MABAYA YA MOYO !
قال العلامة ابن عثيمين- رحمه الله-:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin -Allah amrahamu-:
إذا رأيت الله أنعم على غيرك بمال أو عِلم أو صحة أو جاه أو أولاد أو غير ذلك فقل: اللهم إني أسألك من فضلك
كما قال عز وجل:
{ وَاسْأَلُوا اللَّهَ مِن فَضْلِهِ ۗ }
سورة النساء :٣٢
Pindi atapoona Allah amemneemesha mwenzako kwa mali au elimu au afya au cheo au watoto au visivyokuwa hivyo ,basi sema (hivi) :
” Ewe Allah hakika mimi nakuomba fadhila zako” ,kama alivyosema Allah- aliyeshinda na kutukuka- :
” Na muombeni Allah fadhila zake “.
.Suratu Nnisaa
أما أن تبقى مغموما محزونا كلما رأيت نعمة من الله على أحد اغتممت، فسوف تحرِق نفسك.
Ama ukabakia hali ya kuwa ni mwenye msongo wa mawazo (hali ya) kuwa ni mwenye huzuni ,kila unapoona neema kutoka kwa Allah juu ya yeyote unapatwa na msongo wa mawazo (ukiwa hivi) utaiunguza nafsi yako .
ﺍﻟﻠﻘﺎﺀﺍﺕ الشهرية-لقاء (٣٩)
Maelezo ya muandaaji :
Usitamani neema fulani maalumu ambayo Allah amemneemesha mtu fulani kwa sababu hili hupelekea husuda , usiumie ,wala usiteseke ,na wala usichukie ukawa na huzuni kwa neema ya mtu fulani ,bali muombe Allah fadhila zake ,muombe akupe kama alivyompa huyo au muombe ziada ya hilo ,kwa sababu Allah -aliyetukuka- ndiye aliyempa huyo mtu hii ziada ,au neema hiyo na hili alilolisema sheikh- Allah amrahamu- la kuwa mtu anakuwa na huzuni na msongo wa mawazo pindi anapomuona mwenzie ameneemeshwa neema fulani hii katika husuda ,na kuna wengine huchukia pindi wanapowaona wenzao wana neema fulani , bila shaka mwenye husuda anateseka na kuadhibiwa hapa hapa duniani kabla ya akhera na huwenda akaugua kwa sababu ya husuda aliyokuwa nayo !, Allah amrahamu yule aliyesema :
وصاحب هذا الخلق معذّب في الدنيا فضلا عن الآخرة ،فهو مُنَغَّص العيش أَبَدَ الآباد،كلما جدّد الله نعمه على من يحسده ..زاده تعبه وحزنه .
Na mwenye tabia hii (ya husuda) ni mwenye kuadhibiwa duniani ukiachilia mbali akhera ,yeye ni mwenye maisha mabaya milele ,kila Allah anapomneemesha neema mpya yule anayemhusudu huzidi kupata tabu na huzuni ..
ومن علاماته : أن لا تطاوعه نفسُه التواضع للمحسود ،ولا يقبل له نصحًا؛ ولا يحب أن ينتفع به أحد ،ولا أن يكثر أتباعه وأشياعه .
Na miongoni mwa alama zake (mwenye husuda) : Ni nafsi yake kutomnyenyekea yule anayemhusudu ,na wala hakubali nasaha zake ,na wala hapendi yeyote anufaike na huyo (anayemhusudu) ,na wala hapendi wafuasi wake ,na wale wanaomfuata waongezeke .
وقد قال ابن الجوزي -رحمه الله- في تفسيره لسورة الفلق – :
Na bila shaka amesema ibn l-Jauz -Allah amrahamu- katika tafsir ya suratul- faraq :
والحسد: أخس الطبائع . وأول معصية عصي الله بها في السماء حسد إبليس لآدم، وفي الأرض حسد قابيل هابيل .
Na husuda : Ni tabia mbaya zaidi ,na maasi ya kwanza kabisa aliyoasiwa Allah mbinguni ni husuda ya Ibilis kwa Adam na katika ardhi (duniani) ni husuda ya Kabili kwa (ndugu yake) Habili .
المصدر : زاد المسير – تفسير سورة العلق .
Ufupi wa yote : Husuda ni gonjwa baya la moyo kwa sababu mwenye tabia hii kana kwamba anapingana na kadari za Allah aliyemkadiria huyo anayemhusudu ! na tiba yake ni kuondoa hali hiyo katika moyo na kumuomba Allah fadhila zake ,akupe zaidi au mfano wa hayo aliyompa huyo mwenzako kwa sababu yeye pekee ndiye mtoaji .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 29, 1442H ≈ Jun 9, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•