Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MALEZI YA WATOTO (NO. 03)
قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.
☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto
يقول ابن القيم – رحمه الله –
Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –
٣- “وينبغي لوليِّه أن يُجنِّبَه الأخذَ من غيره غايةَ التجنُّب؛ فإنه مَتى اعتاد الأخذَ صار له طبيعةً، ونشأ بأن يأخذ لا بأن يُعطيَ، ويُعوِّدَه البذلَ والإعطاء، وإذا أراد الوليُّ أن يعطي شيئًا أعطاه إياه على يده؛ ليذوق حلاوة الإعطاء”؛ .
3 – Na inatakikana kwa mlezi wake huyo (mtoto) amuepushe (mtoto) kuchukua kutoka kwa mwenzake ukomo wa kumuepusha, na bila shaka muda atakapozoea kuchukua (kupokea) itakuwa kwake ni tabia,
Na atakulia (atakuwa ni mtu) wa kupokea na si wa kutoa,
Na amzoeshe kujitolea na kutoa,
Na pindi mlezi atakapotaka kumpa chochote (mtoto) ampe kwa mkono wake ili aonje utamu wa kutoa.
📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)
[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Muepushe mwanao na tabia ya kupokea kupita kiasi kwa sababu hilo husababisha kuzoea na matokeo yake anakuwa ni mtu wa kupokea tu na si mtoaji, bali unatakiwa umlee mtoto juu ya tabia ya kutoa sadaka,
Mfano; unaweza ukampa mtoto kiasi fulani akampa mmoja katika mafakiri na wasiojiweza au ukampa pesa akatoe sadaqa mbalimbali zinazochangishwa , na unapompa kitu mtoto mkabidhi katika mkono wake kwa sababu unapofanya hivyo unamuonjesha ule utamu wa kutoa na utaibakisha athari ya hilo katika moyo wake itakayothihiri ukubwani mwake , na atapofikia umri wa kufahamu muelezee faida za kutoa na kumshajiisha katika hilo kwa kumtajia malipo yake mfano ukamsomea hadith hii:
” كل امرئ في ظل صدقته حتى يقضى بين الناس “
“ Kila mtu atakuwa katika kivuli cha sadaqa yake (siku ya kiama) mpaka kutakapohukumiwa baina ya watu ”.
Muelezee mwanao kwa ufupi jinsi sadaka itakavyomnufaisha mtu siku ya kiama! Siku ambayo jua litasogezwa na kuunguza kupita kiasi, na katika amali itakayomsaidia mtu ni sadaka.
Itaendelea … 🖋 Allah akitaka .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa:January 4,2020 na ikarudiwa tena Dhul-Qaadah 11, 1442H ≈ Jun 21, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•