https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MALEZI YA WATOTO (NO. 04)
قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.
☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto
يقول ابن القيم – رحمه الله –
Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –
٤- “ويُجنِّبُهُ الْكَذِبَ والخيانة أعظمَ مما يُجنِّبُه السُّمَّ الناقع؛ فإنه متى سَهَّل له سبيل الكذب والخيانة، أفسَدَ عليه سعادة الدنيا والآخرة، وحَرَمه كلَّ خير”؛
4 – Na (mzazi/mlezi) amuepushe (mtoto) na uwongo na khiyana zaidi ya (vile) anavyomwepusha na sumu kali yenye kuua, basi hakika hali ilivyo muda wowote (mzazi/mlezi) atakapomuwepesishia njia ya uwongo na khiyana (njia hiyo) itamharibia utulivu /raha ya dunia na akhera na itamzuia na kila kheri.
📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)
[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Uwongo ni tabia mbaya na ni katika sababu za kuingia motoni na ni katika matendo ya kinafiki! Na uwongo ni “ Kueleza jambo hali ya kuwa unajua kuwa huu ni uwongo au dhana yako yenye nguvu inamwambia kuwa huu ni uwongo ”.
Kwa hiyo mzazi kuwa na tahadhari na mwanao asiwe na tabia hii chafu na jiepushe na uwongo wewe binafsi usiongope kwa sababu yeye anajifunza kwako, na uwongo hauna utani wala masihara!
Mfano mtume – swala na salamu za Allah zimfikie amesema:
” من قال لصبي :تعال هاك، ثم لم يعطه شيئا فهي كذبة “
“ Mwenye kumwambia mtoto: Njoo (chukua) kisha (akawa) hakumpa chochote basi huo ni uwongo ”.
Mzazi kuwa makini kwa maana unapomuita mtoto na kumdanganya kwa kumpa kitu fulani utakuwa umepata hasara mbili; ya kwanza ni uwongo ulioufanya, na yapili ni kumfundisha mtoto uwongo,
Na jambo la pili ambalo linatakiwa liepushwe kwa mtoto ni khiyana, khiyana ni katika sifa za wanafiki pia, na khiyana ni kwenda kinyume na uaminifu na kuchunga amana mfano mtu akaaminiwa juu ya nafsi au mali au heshima lakini yeye akafanya khiyana kwa maana akavunja uaminfu wake mfano aliachiwa mali akala, au siri akaitoa n.k,
Na hizi ni dhambi ambazo mfanyaji wake anaanza kupata mateso na shida hapa hapa duniani kabla ya akhera.Kwa sababu watu wenye tabia hizi huchukiwa na watu na kutoaminiwa hapa ulimwenguni .
Mwisho: Tuwalee watoto wetu juu ya ukweli na uaminifu hata akifanya kosa mjenge tabia ya kukiri kosa na kama akisema uwongo basi mfahamishe au ikibidi muadhibu kwa huo uwongo.
Itaendelea … 🖋 Allah akitaka .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Iliandaliwa January 7,2020 ,ikarudiwa tena Dhul-Qaadah 12 1442H ≈ June 22, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•