MALEZI YA WATOTO (NO.7)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/Darasazandoa

MALEZI YA WATOTO (NO. 07)

قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.

☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto

يقول ابن القيم – رحمه الله –

Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –

٧ – ويجنبه لبس الحرير فإنه مفسد له ومخنث لطبيعته كما يخنثه اللواط،
وشرب الخمر والسرقة والكذب
وقد قال النبي – صلى الله عليه وسلم –
” يحرم الحرير والذهب على ذكور أمتي وأحل لإناثهم “
والصبي وإن لم يكن مكلفا فوليه مكلف لا يحل له تمكينه من المحرم،
فإنه يعتاده ويعسر فطامه عنه،
وهذا أصح قولي العلماء،

7 – Na (mzazi/mlezi) amuepushe (mtoto) na kuvaa (nguo za) hariri na bila shaka hiyo (hariri) ni yenye kumharibu na ni yenye kuifanya tabia yake kuwa ya kike kama vile liwati inavyomfanya awe na tabia ya kike,
na (amuepushe) na kunywa pombe na wizi na uwongo,
Na bila shaka amesema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – :

“ Ni haramu (mavazi) ya hariri na dhahabu kwa wanaume wa umati wangu na vimehalalishwa kwa wanawake wao ”.

Na mtoto hata kama hakuwa (hakufikia) umri wa kuandikiwa dhambi basi msimamizi wake ni mwenye kuandikiwa dhambi , si halali kwake kumwezesha (kufanya) haramu,
basi bila shaka (mtoto) hulizoea hilo (jambo la haramu) na huwa vigumu kuliacha,
Na hii ni kauli sahihi zaidi ya wanachuoni katika kauli mbili,

واحتج من لم يره حراما عليه،
بأنه غير مكلف فلم يحرم لبسه للحرير كالدابة وهذا من أفسد القياس،
فإن الصبي وإن لم يكن مكلفا،
فإنه مستعد للتكليف،
ولهذا لا يمكن من الصلاة بغير وضوء ولا من الصلاة عريانا ونجسا،
ولا من شرب الخمر والقمار واللواط.

Na ametolea hoja yule ambaye hakuona kuwa ni haramu juu ya huyo (mtoto kuvaa hariri na dhahabu)
Kwamba huyo (mtoto) hakufukia umri wa kuandikiwa dhambi na (Allah) hakumharamishia kuzivaa (nguo za) hariri kama vile (ilivyokuwa si haramu kwa) mnyama kuvishwa vitu hivyo, na hiki (kipimo walichotumia) ni katika vipimo vibaya,
na bila shaka mtoto hata kama hakuwa ni mwenye kuandikiwa dhambi
basi bila shaka ni mwenye kuandaliwa kwa kuufikia umri wa kuandikiwa dhambi,
Kwa ajili hii hawezeshwi/hapewi nafasi ya kuswali bila ya udhu wala kuswali hali ya kuwa yupo uchi na hali ya kuwa ana najisi,
Na wala hawezeshwi/hapewi nafasi ya kunywa pombe na kucheza kamari na liwati.

📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٦٠)

[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa:160) ]

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Nguo ya hariri ni aina fulani ya nguo inayotengenezwa na nyuzi fulani zinazotokana na mdudu anayeitwa nondo wa hariri, nguo hizi ni haramu kwa mwanaume ama kwa mwanamke anaruhusiwa kuvaa , hili ni maalumu kwa mwanamke basi ni haramu kwa mzazi wa kiislamu kumzoesha mtoto wake wa kiume kuvaa vazi hili na mavazi mengine ambayo ni ya kike, ama hariri inayotengenezwa kiwandani hii inaruhusiwa kuvaliwa lakini baadhi ya wanachuoni wanaona bora kujiepusha nayo,

Na wazazi wengi huzembea katika upande huu, unaweza ukamuona mzazi wa kike anamvisha mwanae wa kiume kanga au kitenge bila ya kujali uharamu wa hilo, kwa hiyo mzazi/mlezi kuwa na tahadhari usimlee mwanao wa kiume kwa tabia za kike kike ukawa ni sababu ya kupotea mwanao.

Na mzazi aondoe dhana ya kuwa huyu mtoto hajafikia umri wa kuandikiwa dhambi bali ajue kuwa huyo mtoto anaandaliwa na anaelekea katika huo umri, na pia yeye mzazi anaandikiwa dhambi kosa lake hilo.

Maana ya umri wa kuandikiwa dhambi ni pale atapokuwa mukallafi,

Mukallafi ni yule aliyebaleghe na mwenye akili.

Itaendelea … 🖋 Allah akitaka .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 15, 1442H ≈ June 25, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *