MTIRIRIKO WA KUJIFUNDISHA ADABU ZA MTUME-SWALA NA SALAMU ZA ALLAH ZIMFIKIE- (NO.13)

Mtiririko/mfululizo wa kujifundisha adabu za Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah zimfikie- .

Makala namba (13)

تحريم الغش في الاختبارات

UHARAMU KUFANYA HADAA ( KUIBIA) KATIKA MITIHANI

، قالَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ

Amesema Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah ziwe juu yake

من غش فليس مني  

” Mwenye kufanya hadaa basi (huyo) si katika mimi”

رواه مسلم (١٠٢)

Maelezo ya mfasiri:

Katika matendo yaliyoharamishwa katika dini yetu na ni katika madhambi makubwa ni kufanya hadaa, na dalili ya kuwa hadaa ni katika madhambi makubwa ni pale aliposema “…si katika mimi ” .

Maana yake mwenye kufanya hadaa hayupo katika njia yangu na mwenendo wangu kwa maana amefanya dhambi kubwa .Na hadaa inaingia katika sehemu nyingi mno mfano hadaa katika mitihani kama wafanyavyo baadhi ya wanafunzi ,hadaa katika biashara ambayo ndiyo sababu ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kusema maneno haya, sababu yake ni hii :
Siku moja Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- alipita karibu na fungu la chakula (linalouzwa) akaingiza mkono wake katika hicho chakula alipotoa vidole vyake vilikuwa vimeloa ,basi akamwambia yule muuzaji : “Kitu gani hiki ewe mwenye chakula ? yule mtu akajibu : Kimenyeshewa na mvua ewe Mjumbe wa Allah ,Mtume akamwambia: kwanini haukiweki (hicho kilicholoa )juu ili watu wakione ….” .

Kisha ndiyo akatamka maneno hayo :

“Mwenye kufanya hadaa si katika mimi ” .

Tanbih:

Kuna hadaa ambayo imeenea sana mitandaoni nayo ni hii :

Kuna baadhi ya watu wanachukua makala za watu wengine na baada ya kuzichukua huondoa nembo na kuandika majina yao !tena Kuna wengine tunawajua ni ndugu zetu katika dini ,hata nakumbuka mmoja wao siku moja alipofanya hivyo watu wakagundua na alipoulizwa alisema :Sikukusudia !, tunawaambia watu hawa wamwogope Allah ,tena cha kushangaza kuna wengine wanawaunga mkono katika hili.

Kama unataka kufanyia tarjama makala tafuta yako lakini usifanye hadaa na khiyana ukachukua makala ya mtu na kubadili baadhi ya meneno kisha ukabandika jina lako !hii ni hadaa .

Mtiririko huu ni wenye kuendelea -Allah akitaka-,usikose makala namba (14)

Muandaaji: fawaidusalafiya.net

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 16, 1442H ≈ June 26, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *