https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
๐ธุขุฏูุงุจู ุนูุดูุฑูุฉู ุงูุฒููููุฌูุฉู ููุฒูููุฌูููุง
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (3):
๐ ุฅููู ูุง ุฃูุชูุง ุงูุฒูุฌุฉ ูุฐู ุงูุขุฏุงุจ ูุฅู ุนููู ู ุซู ู ุง ุนูู ุงูุฒูุฌ ู ู ุญููู ููุงุฌุจุงุช ูุญุณู ุนุดุฑุฉ , ูู ู ุฐูู :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
๐ธ
ูฃ- ูุง ุชูุน ุนููู ู
ูู ุนูู ูุจูุญ ููุง ูุฑุงู ุฅูุง ูู ูู ู
ููุญ.
3- ๐ธLisikuone jicho lake katika ubaya na wala asikuone isipokuwa katika uzuri /urembo .
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi -anataja adabu ya tatu katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni hii : Mke anatakiwa ajiweke katika hali ya kumfurahisha mumewe,awe kila anapomuona anafurahi kwa kushikamana kwake na dini,kwa uzuri wake wa tabia,kwa kujipamba /kujiremba kwake ,na hii ni sifa miongoni mwa sifa za mwanamke mwema kama ilivyothibiti kuwa Mtumbe -swala na salamu za Allah zimfikie- aliulizwa : Ni yupi mwanamke bora ?
akajibu:
ุงูุชู ุชุณุฑููู ุฅุฐุง ูุธุฑ ุ ูุชุทูุนูู ุฅุฐุง ุฃู ุฑ ุ ููุง ุชุฎุงูููู ูู ููุณููุง ูู ุงููุง ุจู ุง ููุฑู
Ni yule ambaye anamfurahisha (mumewe) pindi anapomtezama,na anamtii pindi anapomuamrisha, na wala hamuasi (mumewe) kwa kufanya machafu ,na wala (hamuasi) katika mali zake (mume) kwa kuzitoa katika yale asiyoyapenda .
ุฃุฎุฑุฌู ุงููุณุงุฆู (ูฃูขูฃูก).
Ufafanuzi wa hadith:
Huyu ndiye mwanamke bora ,hazina ya mume katika dunia na ndiyo starehe yake bora na ndiye mbora wa wanawake ,na ndiye mwenye baraka kwa mumewe ,na hizo zilizotajwa ni miongoni kwa sifa zake kama vile kumfurahisha mumewe kidini ,kitabia na kimuonekano, kama tulivyoeleza hapo juu na pia katika tabia zake ni kutotoa mali za mume katika yale asiyoyapenda au ya haramu ,na wala hamuasi mumewe kwa kutoka nje ya ndoa yaani kufanya machafu
Tanbih:
Bila shaka uzuri wa kwanza kabisa unaokusudiwa ni uzuri wa dini lakini haina maana mwanamke ajiweke katika hali mbaya kwa mumewe bali anatakiwa ajipambe na kutilia umuhimu usafi na kujipamba ,hebu tumwangalie huyu mmoja katika wema waliopita pindi alipokuwa akimuusia binti yake pindi alipomuozesha :
ูู ู ุง ูุฑูู ูู ูุตูุฉ ุงูุฃุจ ุงุจูุชู ุนูุฏ ุงูุฒูุงุฌุ ู ุง ุฑูุงู ุณุนูุฏ ุจู ูุฒูุฏ:
Miongoni mwa yale yanayopokewa katika wasia wa baba kwa binti pindi anapoolewa ni ule (wasia) alioupokea Sa’iid bin yaziid:โ
ุฃู ุฃุจุง ุงูุฃุณูุฏ ุงูุฏุค ูู ุฒูุฌ ุงุจูุฉ ููุ ูุฃุชุชู ุงูุฌุงุฑูุฉุ ููุงูุช:
ูุง ุฃุจูุ ุฅูู ูู ุฃูู ุฃุญุจ ุฃู ุฃูุงุฑููุ ูุฃู ุง ุฅุฐุง ุฒูุฌุชูู ูุฃูุตููุ ููุงู:
ุฅูู ูู ุชูุงู ู ุง ุนูุฏู ุฅูุง ุจุงููุทูุ ูุงุนูู ู ุฃู ุฃุทูุจ ุงูุทูุจ ุงูู ุงุก.
โKwamba Abuu Al-aswad Addualiy alimuozesha binti yake (basi) yule binti akamjia (baba yake) na akasema:โ
Ewe baba yangu hakika mimi nilikuwa sipendi kuachana na wewe, na ama ukiniozesha (basi) niusie,โ akasema (baba yake):โ
โHakika wewe hauto yapata yale yaliyopo kwake (mume) isipokuwa kwa (kutumia) upole (ulaini), na tambua kwamba manukato mazuri zaidi (ni) maji.โ
(ุนุฒุงู ุงุจู ุงูุฌูุฒู ูู ” ุฃุญูุงู ุงููุณุงุก” (ุต:219) ุฅูู ุงุจู ุฃุจู ุงูุฏููุง ุจุณูุฏ ุตุญูุญ.)
Ufafanuzi :
โMke anatakiwa awe mpole na mlaini kwa mumewe na akiwa hivi basi atapata heri nyingi na kufurahi katika ndoa yake, pia mke atilie umuhimu sana kuusafisha mwili wake kwa kuoga ili mume asimchukie kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka katika mwili wakeโ, kuna baadhi ya wanawake kutokana na kutotilia umuhimu usafi husababisha waume zao kuwachukia ,na pengine ikawa ndiyo sababu ya kutafuta mke mwingine ili apate utulivu, au wale wasiokuwa na hofu ya Allah huingia katika uzinifu ! -Allah atukinge na hilo- ,kwa hiyo ewe mke jitahidi ujiweke katika hali ya kuvutia kwa mumeo usije ukawa ni sababu ya kuharibu ndoa yako .
ุฃุนุฏู :
๐ ุงูุดูุฎ ุฃูุญูู ูุฏู ุจููู ู ูุจูุงุฑููู ุจููู ููุฐูููุงูู ุงููู ูุฒูุฑูููุนููู- ุญูุธู ุงูููู-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
๐๐๐๐๐
Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: โ
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: โ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
๐๏ธ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 16, 1442H โ June 26, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: ๐๐พ
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
โขโโโโโขโฟโโฟโขโโโโโข