ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.5)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (5):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

🌸
٥- أولادك تربيتك فإنه يراك من خلال تربيتك فحسن تربيتك دليل حسن عشرتك.

5- Watoto wako ni malezi yako ,na bila shaka huyo (mume) anakuona kupitia malezi yako ,basi uzuri wa malezi yako ni dalili ya uzuri wa kuishi kwako kwa wema (na mumeo).

Maelezo ya mfasiri:

Sheikh Allah -amuhifadhi- anataja adabu ya tano katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni malezi ya watoto : Anatakiwa mke atambue kuwa pindi anapowasimamia vizuri wanae katika malezi basi hilo humfurahisha mume na huko pia ni katika kuishi vizuri na mume ,na kuzidisha mapenzi ya mume kwake ,na hapa kuna haja ya kutaja baadhi ya nukta zitakamzo msaidia mwanamke -kwa idhini ya Allah – katika kuwalea watoto wake malezi sahihi :

1- Mke anatakiwa ajue kuwa yeye ni mama wa watoto na yeye ndiye msingi katika malezi, kwa sababu yeye mara nyingi huchanganyika na watoto kwa hiyo hupata fursa ya kuwaongoza ,kuwanasihi n.k.

2- Mke anatakiwa ajue yanayowajibika katika malezi na namna ya kuwalea watoto .

3- Soma historia za wanawake wema waliopita ili ujue namna walivyolea watoto wao mpaka wakafanikiwa kuwatoa wanachuoni wakubwa walioijaza dunia elimu ,na maadili mema .

4- Ifanye shughuli hii ya malezi ndiyo mradi wako unaokushughulisha na utoe juhudi zako zote katika hilo, weka mipango mbalimbali katika malezi kwa sababu kuwalea kwako watoto wako katika malezi sahihi ni sadaka yenye kuendelea baada ya kufa kwako.

5- Kithirisha kuwaombea dua na rudia rudia usichoke na haswa zile nyakati ambazo hutarajiwa zaidi kujibiwa dua huwenda dua ikawa ndiyo sababu ya kufaulu katika malezi yako , na kuwaombea dua watoto ni kawaida ya mitume kuwaombea dua watoto wao ,na miongoni mwa dua za nabii Ibrahimu ni hii:

وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَنْ نَعْبُدَ الْأَصْنَامَ”

“Na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu ” .

6- Na katika majukumu yako makubwa zaidi ni kuwatamkisha watoto na kupandikiza itikadi sahihi, na hata kama hawajafahamu katika umri huo baadae watafahamu ,kama vile kuwatamkisha tamko la tauhid :

«لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ ”

Hukuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah .

Na kuwatamkisha maswali matatu ambayo ni katika misingi ya itikadi :

مَنْ رَبُّك، وما دينك ،ومن نبيك .

Nani muabudiwa wako ,na ipi dini yako,na nani Mtume wako ? .

7- Tambua kuwa kipindi cha utoto ni kipindi cha kupandikiza ,na kile kinachopandikizwa muda huo ndicho kitachodhihiri baadae ukubwani kwa hiyo kuwa ni kiigizo chema kwa watoto wako kwa sababu watoto huiga kila wanachokiona .

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

🍃🍂🍃🍂🍃

Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 18, 1442H ≈ June 28, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *