Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا
ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (7):
💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
🌸
٧- إياك وإفشاء سره فإن أفشيت سره لم تأمني غدره وضيق صدره.
🌸
7- Tahadhari na kusambaza siri zake (mumeo), basi kama utasambaza siri zake hautopata amani kutokana na khiyana yake,
na dhiki/uzito wa kifua chake .
🍃🍂🍃🍂
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya saba katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni adabu ya kutunza siri za mume yaani kutunza siri za ndoa na huu ni wajibu kwa mume na mke , na mke pindi atapokuwa anatoa siri za mumewe ajue kuwa kufanya kwake hivyo ni sababu ya kumfanya kuondoa uaminifu wake kwa mumewe na huwenda mumewe akamfanyia khiana kwa sababu ya kueneza kwake siri za ndani ,na pia jambo hilo la kueneza siri za mume humfanya mume kutokuwa na raha na huhisi dhiki katika kifua chake kwa sababu huhisi kila anapopita habari zake zinajulikana! .
Na hukumu ya kutoa siri ndani za baina ya wanando wawili na haswa zinazohusu kitandani ni haramu, na hata siri nyingine kama mume atamwambia asizitoe na kuzieneza au akijua tu kwamba hili mume wake hataki alifahamu yeyote ,na uharamu wa kusimulia ya kitandani umethibiti katika hadithi ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- pale alipowauliza baadhi ya waislamu je kuna yeyote anayefanya jambo hilo yaani anayekutana na mumewe au mume na mkewe kisha anasimulia ? ,baada ya kujibiwa kuwa wapo wanaolifanya hilo ,Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- akasema -:
: هَلْ تَدْرُونَ مَا مَثَلُ ذَلِكَ؟ فَقَالَ:
Je munajua upi mfano wa huyo (mfanyaji wa hilo) ? akasema:
إِنَّمَا مَثَلُ ذَلِكَ مَثَلُ شَيْطَانَةٍ لَقِيَتْ شَيْطَانًا فِي السِّكَّةِ فَقَضَى مِنْهَا حَاجَتَهُ وَالنَّاسُ يَنْظُرُونَ إِلَيْهِ
Hakika si vinginevyo mfano wa huyo ni mfano wa Shetani wa kike aliyekutana na Shetani wa kiume barabarani ,na akakidhi haja zake kwa (huyo Shetani wa kike) na hali ya kuwa watu wanamtezama.
رواه أبو دادد ٢١٧٤
Ufafanuzi wa hadithi:
Hii na dalili wa uharamu wa kutoa siri za kitandani baina ya wanandoa wawili na yale yote yanayohusu tendo la ndoa ,na dalili ya uharamu wa hilo ni pale Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- amemweka mtu huyu katika daraja la mashetani wanaoingiliana na watu wanawatezama ! .
Na hadithi nyingine inayojulisha uharamu wa hilo ni kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- :
( إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللَّهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى امْرَأَتِهِ وَتُفْضِي إِلَيْهِ ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا ) .
{Hakika katika watu wenye daraja baya zaidi mbele ya Allah siku ya kiama ni mwanamume anayekutana na mkewe na (mke) akakutana na yeye kisha akaeneza siri yake } .
رواه مسلم ( ١٤٣٧ ) .
Mchanganuo wa hadithi:
Hii ni dalili kuwa ni haramu kuadithia mambo yanayotokea baina ya wanandoa na hapa ametajwa mwanaume kwa sababu mara nyingi hili hutokea kwa wanaume kama walivyoeleza baadhi ya wanachuoni .
Na aliulizwa sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
Inazidi kwa baadhi ya wanawake (tabia ya) kuhamisha mazungumzo ya ndani na maisha yao ya ndoa pamoja na waume zao (huyapeleka) kwa ndugu zao na rafiki zao ,na baadhi ya haya mazungumzo ni siri za ndani (ambazo) waume hawapendi kuyajua yeyote ,basi ni ipi hukumu juu ya wanawake ambao hufanya tendo la kueneza siri na kuzihamisha nje ya nyumba au kwa baadhi ya wanafamilia ?
Sheikh akajibu kwa kusema:
إن ما يفعله بعض النساء مِن نقل أحاديث المنزل والحياة الزوجية إلى الأقارب والصديقات أمر محرَّم ، ولا يحل لامرأة أن تفشي سرَّ بيتها ، أو حالها مع زوجها إلى أحدٍ من الناس ،
Hakika yale wanayoyafanya baadhi ya wanawake katika kuhamisha baadhi ya mazungumzo ya nyumbani na maisha ya ndoa kwa ndugu na marafiki (hili) ni jambo la haramu ,si halali kwa mwanamke kueneza siri za nyumbani kwake au hali yake pamoja na mumewe kwa yeyote katika watu ,
قال الله – تعالى – : ( فالصالحات قانتات حافظات للغيب بما حفظ الله ) ،
amesema Allah -aliyetukuka-:
{Basi wanawake wema ni wale wenye kudumu na kumtii .(Allah) ,wanaojihifadhi (hata) wasipokuwepo (waume zao); kwa kuwa Allah amewaamrisha wajihifadhi .
وأخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن ( شر الناس منزلة عند الله يوم القيامة الرجل يفضي إلى المرأة وتفضي إليه ثم ينشر سرها ) .
na ameeleza Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- kuwa :
{Mtu mwenye daraja baya zaidi mbele ya Allah siku ya kiama na mwanamume anayekutana na mwanamke (mkewe) ,na (mwanamke) akakutana na mumewe kisha akaeneza sira zake } .
” فتاوى إسلامية ” (٢١٢،٢١٣/١٣)
Tanbih:
Haifai kuelezea kwa wanandoa kutoa siri za kitandani ila kukihitajika hilo kama vile mbele ya Kadhi .
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
🍃🍂🍃🍂🍃
Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 21, 1442H ≈ Jul 1, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•