https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا
ADABU ZA MKE KUISHI NA MUMEWE.
Makala namba (8):
💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :
Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :
🌸
٨- زوجك جنتك أو نارك فحسن العشرة وجميل الصحبةوحسن الكلمة تضمن لك تلك الجنة.
🌸8- Mume wako ni pepo yako au moto wako ,basi ishi naye kwa wema,na suhubiana (kuwa) naye kwa uzuri ,na kwa maneno mazuri, (matendo hayo) yatakudhaminia pepo .
🌸
🍃🍂🍃🍂🍃
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amuhifadhi-anataja adabu ya nane katika adabu za mke kuishi na mumewe nayo ni hii ambayo ni kama vile inatilia nguvu adabu zilizopita nayo ni kuwa mke anatakiwa aishi na mume wake kwa wema mpaka mumewe amridhie , na ajiepushe na kumuudhi mumewe kwa sababu huyo mume ndiyo pepo yake au moto wake!, ni nini maana ya maneno haya tusome hadithi hii :
وروى الإمام أحمد والحاكم عن الحُصَيْن بن مِحْصَن:
Amepokea imamu Ahmad na Al-hakim kutoka ka Al-huswain bin Mihswan :
أن عمة له أتت النبي -صلى الله عليه وسلم- في حاجة ففرغت من حاجتها، فقال لها النبي -صلى الله عليه وسلم-:
Kuwa shangazi yake alimjia Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kwa ajili ya haja (fulani), alipomaliza haja yake, Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- akamuuliza :
“أذات زوج أنت”؟ قالت نعم. قال:”كيف أنت له؟” قالت: ما آلوه (أي لا أقصّر في حقه) إلا ما عجزت عنه.
” Je una mume ” ? ,akajibu:Ndio .(Mtume) akamuuliza (tena) : Upo naye vipi ?, akajibu: Sipunguzi katika haki zake isipokuwa yale niliyoyashindwa .
قال:”فانظري أين أنت منه فإنما هو جنتك ونارك”.
(Mtume) akasema: Basi angalia /chunguza upo naye vipi huyo (mumewako) ,na hakika si vinginevyo huyo (mume ni) pepo yako na moto wako .
[قال الهيثمي في مجمع الزوائد(٥٦٣/٤):”ورجاله رجال الصحيح خلا حصين وهو ثقة”.
Kauli yake Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- :
“…Hakika si vinginevyo huyo (mumeo) ni pepo yako na moto wako ” .
Maana yake : Huyo mume ni sababu ya kuingia mke peponi kama akitekeleza haki zake na mume akafurahi na kumridhia mkewe hiyo ni sababu ya kuingia peponi ,na ni sababu ya kuingia kwake motoni kama akizembea katika hilo kama vile akamkasirisha na kumfanyia ujeuri n.k.
Mke ajitahidi katika kumtii na kumridhisha mumewe katika yale ya halali awe karibu na mumewe katika dhiki na raha aitikie wito wake pindi anapomuhitaji, akiishi hivi na mumewe basi ni sababu ya kuingia peponi , na vile vile atahadhari na kumuasi mumewe na kutomtekelezea haki zake kwa sababu kufanya hivyo ni katika sababu za kuingia motoni, na kwa hadithi hii baadhi ya wanachuoni wameeleza kuwa kumuasi mume na kumfanyia jeuri ni katika madhambi makubwa .
TAHADHARI:
Wanawake wengi wameacha kuwaheshimu na kuwakirimu waume zao na kuchunga haki zao ni kwa sababu ya kuathirika kwao na maneno ya makafiri wa kimagharibi ya kudai usawa baina ya jinsia mbili yaani wanaume na wanawake, au kauli yao:Mwanamke anaweza ! ,wanakusudia kuwa anaweza kusimamia yale majukumu ya mwanamume !.
Wanawake wa kiislamu washikamane na dini yao ambayo miongoni mwa mafundisho yake ni mke kumtii mume ,na kumuheshimu na kumpa nafasi yake ya usimamizi wa nyumba akiwemo yeye mke.
أعده :
🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-
Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .
🍃🍂🍃🍂🍃
Tarjama na maelezo : fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 23, 1442H ≈ July 3, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•