MISINGI MITATU NA DALILI ZAKE (NO.12)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

📖 ثلاثة الأصول و أدلتها 📖

Misingi mitatu na dalili zake.

makala namba ( 12)

🌱والرب هو المعبود🌱

Na Mola Mlezi yeye ndiye muabudiwa.

↩والدليل قوله تعالى:

{{ يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُواْ رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ.

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الأَرْضَ فِرَاشاً وَالسَّمَاء بِنَاء وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاء مَاء فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ فَلاَ تَجْعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ }}

Na dalili ni kauli yake (Allah) aliyetukuka:

{Enyi watu muabuduni Mola wenu Mlezi ambaye amekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kumcha (Allah).

(Mola Mlezi ambaye) amekufanyieni ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa,na akateremsha maji kutoka mawinguni,na kwa hayo (maji) akatoa matunda ni riziki kwenu. Basi msimfanyie Allah washirika ,na hali nyinyi mnajua (kuwa hana mshirika).

🌱قال ابن كثير رحمه الله تعالى :

الخالق لهذه الأشياء هو المستحق للعبادة

Amesema ibn Kathiir Allah aliyetukuka amrehemu:

“muumba wa vitu hivi ndiye anayestahiki kuabudiwa.

Maelezo mfasiri yanayotokana na sherehe za wanachuoni :

Shekh Allah -amrehemu- aliposema Mola mlezi ndio muabudiwa akakusudia kuwa yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa pekee na haitoshelezi kwa mtu kukiri kuwa Allah ndiye Mola Mlezi na muumba wa kila kitu bali ni lazima kukiri kuwa Allah pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa na amtakasie ibada kwa maana amuabudie yeye pekee.

Na katika hii aya Allah-utakasifu ni wake – anawaita watu wote :Waumini (waislamu) ,Makafiri, Wanafiki ,kwa hiyo katika aya hii tumeona kuwa watu wamegawanyika vigawanyo vitatu:

1-Waumini ambao katika sifa zao wanayaamini yale yasiyoonekana ambayo ameyaeleza Allah na Mtume wake, ,na wanaamini siku ya mwisho,na watu hawa Allah amewasifu kuwa ndio wenye kufaulu

2- Makafiri ambao ni wapingaji na hawa ni wale wanaodhihirisha ukafiri na kupinga.

3- Wanafiki ambao hawako pamoja na Wauminini na wala hawakopamoja na Makafiri na hawa ni wale ambao hudhihirisha kuwa ni Waumini (waislamu) na huficha ukafiri katika nyoyo zao na watu hawa ni wabaya zaidi kuliko Makafiri,kwa sababu hii Allah ameteremsha aya nyingi kuhusu Wanafiki kuliko aya za Waumini na Makafiri.

Wanachuoni wameeleza kuwa :

Wito wa kwanza katika msahafu ni huu :

{Enyi watu muabuduni Mola wenu Mlezi} na hii aya emekusanya amri ya kumuabudia Allah na kumtakasia Allah katika ibada na hii ni amri ya kwaza katika msahafu kwa hiyo hapa tunapata faida kuwa amri ya kwanza katika msahafu ni amri ya tauhid. yaani kumpwekesha Allah katika ibada.

Kisha sheikh -Allah amrahamu- akaleta maneno ya ibn Kathir- Allah amrahamu- yanayotafsiri hiyo aya kwa maana anayestahiki kuabudiwa ni huyu aliyeyafanya haya yote : Aliyeumba,anayeruzuku,aliyeifanya ardhi kuwa ni tandiko ,anayeteremsha mvua kutoka mawinguni.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 24, 1442H ≈ July 4, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *