TAKBIRA ZINAANZA LINI KATIKA MASIKU KUMI YA MWANZO YA MWEZI WA DHUL-HIJJAH ?

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

متى يبدأ التكبير المطلق في شهر ذي الحجة ؟

Ni lini zinaanza takbira zisizofungwa na muda wala sehemu ktk mwezi wa Dhul-hijjah (Mfungo tatu) ? .

يبدأ التكبير المطلق.
في عشر ذي الحجة:
من دخول ذي الحجة،
أي من غروب شمس آخر يوم من شهر ذي القعدة،
إلى آخر يوم من أيام التشريق،
وذلك بغروب شمس اليوم الثالث عشر من شهر ذي الحجة.

Zinaanza takbira
zisizofungwa /na muda wala sehemu ,
Katika siku kumi za mwezi wa mfungo tatu:

Tokea unapoingia (mwezi) wa mfungo tatu,

Yaani kuanzia kuzama kwa jua ya siku ya mwisho katika mwezi wa mfungo pili,

Mpaka siku ya mwisho katika masiku ya kukausha nyama,

Na (inaisha) siku hiyo kwa kuzama kwa jua kwa siku ya kumi na tatu katika mwezi wa mfungo tatu.

انظر: مجموع فتاوى الشيخ ابن باز ١٧/١٣، الشرح الممتع للشيخ ابن عثيمين (٢٢٠/٥)

Angalia :

Maj’muu fatawaa ya Sheikh Ibn Baaz (13/17), Assher’he l-mumti’i cha Ibn ‘Uthaimin (5/220) ]

Maelezo ya mfasiri – Allah amuhifadhi

Masiku haya kumi ya mwazo ya mfungo tatu (dhul-hijjah) yanafadhila na ubora mkubwa tunatakiwa tukithirishe kufanya ibada mbalimbali na katika ibada bora katika masiku haya ni kumtaja Allah kwa kuleta takbira na tahliil na tasbiih.

الله أكبر الله أكبر لا إله إلا الله و الله أكبر ، الله أكبر ولله الحمد.

Na hizi takbira zilizoachwa huru yaani zisizofungwa na wakati wala sehemu bali anatakiwa kila sehemu na kila wakati muislamu akithirishe kumtaja Allah isipokuwa zile nyakati ambazo haruhusiwi kumtaja Allah ,kama vile wakati wa kujisaidia,ndani ya tendo la ndoa,wakati anaposikiliza khutba ya ijumaa,na anapokuwa ndani ya swala .

Ama takbira zilizofungwa na muda zinaanza baada ya swala ya alfajiri ya siku ya Arafa na zinaletwa kila baada ya swala baada ya salamu tu na zinamalizika baada ya swala ya alasiri ya tarehe 13 ya Dhul-Hijjah (Mfungo tatu).

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa August 3, 2019M, ikarushwa tena Dhul-Hijjah 1, 1442H ≈ Jul, 11, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. mohamedi majid

    اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎
    allah awajaze kheri nyngi na subira katika kusambaza elimu hii ya dini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *