NITANGULIZE KULIPA DENI AU KUCHINJA UDH’HIYAH ?

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

NITANGULIZE KULIPA DENI AU KUCHINJA UDH’HIYAH?

سئل العلامة ابن عثيمين – رحمه الله –

Aliulizwa mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin –

ما حكم الأضحية إذا كانت بدين مؤجل ؛ هل تجزئ أو لا بد من الاستئذان من صاحب الدين؟

Ipi hukumu ya kuchinja udh’hiyah ikiwa (mtu) ana deni la baadae, je itafaa kwake au hakuna budi kumtaka idhini anayemdai?

الجواب:

Jawabu:

لا أرى أن يضحي الإنسان وعليه دين إلا إذا كان الدين مؤجلاً، وهو عالم من نفسه أنه إذا حل الدَّيْن تمكن من وفائه، فلا بأس أن يضحي، وإلا فليدخر الدراهم التي عنده للدَّيْن،

Sioni kuwa mtu achinje hali ya kuwa juu yake kuna deni ila likiwa deni ni la baadae na hali ya kuwa anajijua kuwa yeye ataweza kulilipa hilo (deni) pindi utakapofika muda wake, basi (katika hali hii) hakuna ubaya wa kuchinja udh’hiyah, na kama si hivyo basi aweke akiba pesa alizokuwa nazo kwa ajili ya deni,

الدَّيْن مهم – يا إخواننا – كان الرسول عليه الصلاة والسلام إذا قدم إليه رجل يصلي عليه ترك الصلاة عليه، حتى إنه في يوم من الأيام قُدِّم إليه رجل من الأنصار فخطا خطوات ثم قال: (هل عليه دَين؟ قالوا: نعم, قال : صلوا على صاحبكم، ولم يصل عليه، حتى قام أبو قتادة رضي الله عنه وقال: الديناران عليَّ, فقال: حق الغريم وبرئ منه الميت, قال: نعم يا رسول الله! فتقدم وصلى)، ولما سئل عن الشهادة في سبيل الله وأنها تكفر كل شيء قال: (إلا الدَّيْن) الشهادة لا تكفر الدَّيْن، فالدَّيْن ليس بالأمر الهين –

deni ni muhimu – enyi ndugu zangu – alikuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – atakapoletewa mtu (aliyefariki ili) amswalie (akiwa na deni) huacha kumswalia , mpaka yeye (Mtume) siku katika masiku aliletewa mtu mmoja katika wenyeji wa Madinah basi akapiga hatua kadhaa kisha akasema:

{ Je (huyu maiti) ana deni? wakajibu: Ndio, akasema: Mswalieni mwenzenu, na (yeye Mtume) hakumswalia, mpaka akasimama Abuu Qatadah – Allah amridhie – na akasema: Hizo dinari mbili nitazilipa mimi, basi akasema (Mtume): Je, deni limehamia kwako na maiti limetoka katika shingo yake?, akajibu (Abuu Qatadah): Ndio ewe Mjumbe wa Allah, basi (Mtume) akatangulia mbele na akamswalia.

Na pindi alipoulizwa (Mtume) kuhusu kufa shahidi katika kuipigania dini ya Allah na kwamba (kifo hicho) kinafuta kila kitu (katika madhambi) akasema (Mtume) { Isipokuwa deni }, kufa shahidi katika jihadi hakufuti deni, basi (itambulike kuwa) deni si kitu chepesi,

يا إخواننا – أنقذوا أنفسكم، لا تصاب البلاد بمصيبة اقتصادية في المستقبل, لأن هؤلاء الذين يستدينون ويستهينون بالدَّيْن سيفلسون فيما بعد، ثم يفلس مَن وراؤهم الذين ديَّنوهم، فالمسألة خطيرة للغاية، وما دام الله عز وجل يسر للعباد العبادات المالية ألا يقوم بها الإنسان إلا إذا كان عن سعة فليحمد الله وليشكر.

Enyi ndugu zangu – ziokoeni nafsi zenu, isije nchi ikapatwa na balaa la uchumi siku za usoni kwa sababu hawa ambao wanaokopa na wanaona madeni ni kitu chepesi watakuja kufilisika baadae kisha watafilisika wale waliopo nyuma yao ambao wamewaingiza katika madeni, basi masuala (ya deni) ni hatari mno, maadamu Allah amewawepesishia waja ibada za mali (haziwajibiki kwao) kuzitekeleza ila (mtu) akiwa na wasaa basi (mja) amsifu Mola wake Mlezi na amshukuru.

اللقاء الشهري (رقم ٥٣، سؤال رقم ٢٤)

[ Alliqaau shahriy (Namba 53, swali la 24) ]

ويقول في “الشرح الممتع” (٤٥٥/٨)

” إن كان عليه دين ينبغي له أن يبدأ بالدين قبل الأضحية “

Na anasema (pia) katika sher’he l-mumti (8/455):

” Akiwa ana deni basi inatakikana yeye aanze kulipa deni kabla ya udh’hiyah “

Maelezo ya muandaaji :

Kulipa deni ni wajibu na udh’hiyah ni suna iliyokokotezwa kwa wanachuoni wengi zaidi na hata wale wanaosema ni wajibu inabakia pale pale kuwa deni la mtu linatangulizwa kwa sababu ni haki ya binadamu, na pia wanaosema udh’hiyah kuwa ni wajibu ni kwa yule mwenye uwezo na mwenye deni haingii katika wenye uwezo,

Unapolipa deni unaiepusha nafsi yako na mzigo uliojibebesha na unaponunua kichinjwa cha udh’hiyah hali ya kuwa una deni ni kuibebesha nafsi mzigo wa deni na deni ni haki ya waja na udh’hiyah ni haki ya Allah iliyosuniwa na haki ya mja inatangulizwa,

Deni ni hatari kwa mja huwenda akafa hali ya kuwa hajalilipa na uwezo anao ikiwa ndiyo sababu ya kugawa mema yake siku ya kiama kwa yule muislamu anayemdai, Isipokuwa anaweza kuchinja katika hali hiyo aliyoitaja Sheikh – Allah amrahamu – yaani muda wa kulipa upo mbali na anajiona kuwa ana uwezo wa kulipa.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa : Dhul-Hijjah ,7-1441H ≈ 28-July-, 2020M, ikarushwa tena :Dhul-Hijjah 1,-1442H =11 Jul,2021

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *