JE UWAHABI UPO ?

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

JE UWAHABI UPO ?

قال العلامة الفوزان – حفظه الله –

Amesema mwanachuoni mkubwa Al-fauzaan – Allah amuhifadhi –

الدولة العثمانية عندهم خرافات،وعندهم أضرحة وعندهم تصوف وبدع .

Serikali ya Al-‘Uthmaaniyyah ina upotevu,
na wana makaburi (yenye kufanywa ushirikina ndani yake ) na wana utwariqah na uzushi,

فخشوا أن دعوة الشيخ محمد بن عبد الوهاب تصلهم في بلادهم،لذلك حاربوا الدولة السعودية .

،basi wakaogopa kuwa ulinganiaji wa Sheikh Muhammad bin ‘Abdil-Wwahhaab utafika katika miji yao (nchi yao),

Kwa ajili hiyo waliipiga vita serikali ya Saudia.

📓 المصدر: الإجابات الفاصلة ص (٣٩)

[ Chimbuko: Al-ijaabaatu l-faaswilah, ukurasa (39) ]

قال العلامة ابن باديس – رحمه الله –

Amesema mwanachuoni mkubwa Ibn Baadiis – Allah amrahamu –

الأتراك هم الذين أطلقوا على حنابلة نجد مسمى (الوهابية)،وهم الذين نشروا عنهم التهم والأكاذيب في العالم الإسلامي

Waturuki wao ndio walio waita Mahanabilah wa Najd jina la (Uwahabi),

Na wao ndio ambao wamewaenezea tuhuma na uwongo katika ulimwengu wa kiislamu,

وأستأجروا الفقهاء في جميع الأقطار ليؤلفوا،ويكتبوا ويكذبوا على حنابلة نجد

Na wakawaajiri wanachuoni katika pande zote za dunia ili watunge (vitabu),
na waandike na wawaongopee Mahanabilah wa Najd.

📓 المصدر: مجلة الصراط عدد (٥)

[ Chimbuko: Majjalatu sswiraat, toleo (5) ]

قال العلامة حماد الأنصاري – رحمه الله –

Amesema mwanachuoni mkubwa Hammaad Al-answaariy – Allah amrahamu –

لم يؤلف وينشر ويطبع ضد الدعوة السلفية أحد في الدنيا مثل تركيا ودولة الروافض في إيران،

Hakuna yeyote aliyetunga na aliyesambaza na aliyechapisha dhidi ya da’awa ya salafiyyah duniani kama (ilivyofanya) Uturuki na serikali ya Mashia Iran,

فإن العقيدة السلفية ما قل انتشارها حتى حكم الأتراك، وهم نقشبندية، والنقشبندية أعداء للعقيدة السلفية.

Na bila shaka itikadi ya wema waliopita haikupungua kuenea kwake mpaka walipo hukumu Waturuki,
nao hao (Waturuki) ni Naqshabandiyah, na Naqshabandiyah ni maadui wa itikadi ya wema waliopita.

📓 المجموع في ترجمته (٦٩١/٢)

[ Al-maj’u’u katika historia yake (2/691) ]

Maelezo kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi

Maadui wakubwa wa tauhidi ni wale wenye kuabudia makaburi miongoni mwa watu wa twariqa mbalimbali kama twariqa ya Naqshaband, na nyinginezo wakishirikiana na Mashia!

Mfano: hapa kwetu Tanzania kuna kitabu kinachoitwa Upotevu wa madhehebu ya “Uwahhab” (Answaru Sunna) kilichotungwa na mmoja wa watu wa twariqa ya qadiriyah anayeitwa Khalifa Khamis Muhammed, bali uhalisia ulivyo tunasema hajakitunga isipokuwa alichofanya ni kuchukua vitabu vya maadui wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhaab – Allah amrahamu – ambao ni maadui wa uislamu sahihi unao waamrisha watu wasimuabudie yeyote isipokuwa Allah,

yeye alichofanya ni kuchukua vitabu vya watu wa twariqa mbalimbali duniani na vya mashia kisha akavileta katika lugha ya kiswahili, na kitabu hiki mashia wamekihudumia vilivyo na kuvigawa buree! ili kutaka kuwapoteza waislamu wasio kuwa na elimu na wanaofuata mkumbo, na hapa utajua jinsi gani Mashia siku zote huwatumia Masufi katika kueneza Ushia .

Faida:

Na serikali ya kiislamu ya Uthmaaniyah wanahistoria wanasema miongoni mwa sababu kubwa ya kuporomoka kwake ni kuupiga vita ulinganiaji wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahhaab – Allah amrahamu ambaye alikuwa akiwalingania watu wampwekeshe Allah na kuachana na ushirikina na hii ndiyo dini waliyokuja nayo mitume wote -amani iwe juu yao-.

Kwa hiyo mtu akisema: Uwahabi upo .

Sisi tunamwambi: Uwahabi ni jina walilolianzisha maadui wa uislamu sahihi ili kuwafukuza watu katika uislamu sahihi ambao aliufundisha Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ,na wanachuoni wema walikuwa wakiuhuisha uislamu huu pindi unapopotea katika jamii, na miongoni mwa wale waliouhuisha uislamu sahihi baada ya kutoweka kwa kiasi kikubwa katika jamii ni sheikh Muhammad bin Abdil-Wahhab -Allah amrahamu- , na sheikh itikadi yake ilikuwa ni ya kisalafi yaani itikadi ya wema waliopita, na madhehebu yake ya kifiqih alikuwa ni hanbaliy ,na wala hukuanzisha madhehebu mapya kama wanavyotangaza maadui .

Kwa hiyo mwenye kusema kuwa Uwahabi upo ,tunamwambia hivi :

Kama unakusudia kuwa kuna watu wenye kukemea ushirikina na uzushi na kupambana na washirikina na wazushi basi watu hawa wapo ama jina hilo munalowaita ni jina walilolibuni maadui wa uislamu wa kweli .

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la kwanza: March 10, 2020M ,toleo la pili Dhul-hijjah 17, 1442H ≈ Jul 27, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *