ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE (NO.13) .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🌸آدَابُ عِشْرَةِ الزَّوْجَةِ لِزَوْجِهَا

ADABU ZA MKE KATIKA KUISHI NA MUMEWE.

Makala namba (13):

💐 إليك يا أيتها الزوجة هذه الآداب فإن عليك مثل ما على الزوج من حقوق وواجبات وحسن عشرة , فمن ذلك :

Chukua ewe mke hizi adabu ,hakika bila shaka kuna haki zinazowajibika kwako kumfanyia mumeo mfano wa zile haki zinazowajibika kwa mume kumfanyia mkewe ambazo ni haki (mbalimbali) na (mambo) ya wajibu , na kuishi kwa wema ,na miongoni mwa hizo (adabu ni) :

💐١٣- كوني معظمة لأمره لا معارضة لطلبه مجادلة لأفكاره, إلا بأساليب لطيفة وإشارات خفيفة؛ لقصد تحقيق الأفضل للحياة الزوجية .

🌸13- Kuwa ni mwenye kuzitukuza amri zake (mumeo na usiwe ni) mwenye kupinga yale anayoyataka,(na usiwe) mwenye kujadiliana na fikra zake ila kwa njia (ya) ulaini na ishara khafifu, kwa makusudio ya kuthibitisha maisha bora ya ndoa .

🍃🍂🍃🍂🍃

Maelezo ya mfasiri:

Sheikh -Allah amuhifadhi- anataja adabu ya kumi na tatu (13) katika adabu za mke katika kuishi na mumewe ,nayo ni adamu ya kuwa mtiifu kwa mumewe ,na kutopinga yale anayoyataka maadamu hayaendi kinyume na sheria ya Allah,na wala asijadiliane na mumewe kwa kubishana naye ila kama itabidi kufanya hivyo basi anatakiwa mke mtumie njia mzuri na ishara ya mbali, na kufanya hivyo ndiyo sababu ya kuimarisha ndoa .

Hebu tujifundishe katika tukio lililotokea katika suluhu ya Hudaibiyah ,baada ya waislamu kuzuiliwa kuingia Makkah kutekeleza ibada ya Umrah , Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-aliwaamrisha waislamu wanyoe na wachinje vichinjwa vyao lakini hakuna yeyote aliyetekeleza hayo waliyoambiwa ,na Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alirudia mara tatu lakini hawakufanya,basi Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- aliingia kwa mkewe Ummu Salamah na akamtajia hilo lililotokea kwa waislamu basi Ummu Salammah -Allah amridhie- akasema:

يا نبي الله، أتحب ذلك اخرج ولا تكلم أحدا حتى تنحر بدنك (ذبيحتك) وتدعو حالقك فيحلقك،

Ewe Nabii wa Allah, je unapenda (watekeleze) hilo, (basi wewe) toka na wala usimsemeshe yeyote mpaka uchinje ngamia wako (kichinjwa chako) na umuite kinyozi wako na akakunyoa,

فخرج رسول الله وفعل بمشورتها فما كان من المسلمين إلا أن نحروا وحلق بعضهم لبعض، وبذلك حلت المشكلة.

basi akatoka Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie- na akaufanyia kazi ushauri wake (Ummu Salamah) ,basi ghafla waislamu wakachinja (vichinjwa vyao) na wakanyoana , na kwa (ushauri wake) ukapatikana ufumbuzi tatizo (hilo).

Faida katika tukio hili:

Hapa tunapata faida kuwa mke anaweza akamshauri mumewe na mume si vibaya kuuchukua ushauri wake bali anatakiwa auchukue ukiwa mzuri ,na vile vile tunajifundisha kuwa mke pindi anapomshauri mumewe anatakiwa atumie njia mzuri ya upole na ulaini na kubembeleza kama alivyofanya Ummu Salamah- Allah amridhie- .

Unajua kwanini unapojadiliana na mumeo unatakiwa utumie njia ya upole,ulaini, na kubembeleza ? .

Kwa sababu mwanamume hapendi kutawaliwa na mwanamke siku zote anapenda awe juu yake kwa hiyo unapotumia ukali,hasira yeye huhisi kuwa unamvunjia heshima na kumdharau na kujiweka juu yake, na hapo hatuchukua ushauri wako , na kama amekosea na ukamkosoa kwa njia hii basi hatojirekebisha .

🍃🍂🍃🍂

أعده :

🖊 الشيخ أَحْمَدُ بْنُ مُبَارَكٍ بْنِ قَذْلَانَ الْمَزْرُوْعِيّ- حفظه اللّه-

Ameiandaa : Sheikh Ahmad bin Mubarak bin Qadhlan Al-Mazru’iy -Allah amuhifadhi .

Tarjama : Ismail Seiph Mbonde .
🍃🍂🍃🍂🍃
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 19, 1442H ≈ Jul 29, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Abuu Rabee MULJIBUL bin MUKANDARA

    Allah akulipeni khayr kwa jitihada zenu katika kuisomesha dini ya Allah.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *