Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU- AMANI IWE JUU YAKE .
Makala namba (17):
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
وَٱسۡتَبَقَا ٱلۡبَابَ وَقَدَّتۡ قَمِيصَهُۥ مِن دُبُرٖ وَأَلۡفَيَا سَيِّدَهَا لَدَا ٱلۡبَابِۚ قَالَتۡ مَا جَزَآءُ مَنۡ أَرَادَ بِأَهۡلِكَ سُوٓءًا إِلَّآ أَن يُسۡجَنَ أَوۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ (٢٥)
Na (wote wawili) wakakimbilia mlangoni,na mwanamke akairarua kanzu yake (Yusuf) kwa nyuma. Na wakamkuta mume wake mlangoni; mwanamke akasema:Hakuna malipo ya mwenye kutaka kufanya ubaya na mkeo isipokuwa kufungwa gerezani au kupewa adhabu inayoumiza .
Suratu Yusuf (25).
Maelezo ya muandaaji:
Yusuf alikimbilia mlangoni ili atoke,na yule bibi naye akamkimbiza ili amzuie kutoka ,yaani kila mmoja alikuwa akikimbia .Na yule mwanamke katika purukushani za kumzuia Yusuf kutoka akaivuta kanzu yake kwa nyuma ili kumzuia ,akaichana.Hapo wakakutana na mume wa yule bibi mlangoni ,na hapa Allah amemuita mume wa huyu bibi kwa jina la “assayyid” /Bwana kwa maana hii ni dalili kuwa mume ndiye msimamizi wa mwanamke kama alivyosema Allah- aliyetukuka:
{الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء}
{Wanaume ni wasimamizi wa wanawake}
النساء ٣٤ .
Lakini haina maana kuwa mwanamume amtese mkewe na kumnyanyasa, huu si usimamizi alioukusudia Allah ,na ndiyo maana Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie amesema hivi:
” …فإنما هن عوان عندكم…”
Basi hakika si vinginevyo hao (wanawake) ni mateka kwenu .
Maana yake: mume atilie umuhimu na pupa katika kumsimamia yale yanayohusu dini yake na dunia yake ni kwa sababu huyo mwanamke yupo chini ya mwanamume, ndiyo maana akafananishwa na mateka na wala haina maana anyanyaswe bali ni wajibu apewe haki zake za kisheria na ndiyo maana Allah amesema:
( وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ )
Na (wanawake) wanayo haki kwa sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao .Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao .
البقرة : ۲۲۸ .
Turudi katika kisa :
Yule mwanamke aliogopa kuwa mumewe anaweza akawatuhumu kwa kufanya machafu akamwambia mumewe kwa kumchongea Yusuf: Hakuna malipo kwa anayetaka kumfanyia mabaya mkeo isipokuwa itiwe gerezani au apitishiwe adhabu iumizayo kwa kuchapwa viboko au mfano wa hiyo ,na wala hakusema kuwa Yusuf auliwe na hilo ni kwa sababu yeye alimpenda Yusuf na mtu hapendi kumuua kipenzi chake ndiyo maana akaashiria afungwe kwa sababu ipo siku atatoka au aadhibiwe kama kupigwa n.k ,adhabu ambazo hazitopelekea kufa .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 19, 1442H ≈ Jul 29, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•