ثمانية أحوال تدعو فيها الملائكة لابن آدم.
٨-الثامن :
HALI NANE (AMBAZO) MALAIKA HUMUOMBEA DUA NDANI YAKE MWANADAMU (NO. 8)
8 – (Hali) ya Nane:
المتسحرين.
☞ Wenye kula daku.
عن ابن عمر رضي الله عنهما:
Kutoka kwa Ibn ‘Umar – Allah awaridhie (yeye na baba yake):
أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
Kwamba Mjumbe wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie – amesema:
« إن الله تعالى وملائكته يصلون على المتسحرين »
“ Bila shaka Allah na malaika wake huwaswalia wenye kula daku ”
📚 صححه الألباني. صحيح ابن حبان ،ومعجم الطبراني الأوسط بإسناد حسن .
[ Ameisahihisha Al-albaaniy ]
Maelezo Kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi
Ubora na fadhila za kula daku unapatika hata kwa yule anayetaka kufunga funga ya sunnah.
Na daku inabaraka na faida nyingi ,hebu tusome maneno ya huyu mwanachuoni :
قال ابن حجر – رحمه الله –
Amesema Ibn Hajar – Allah amrahamu –
البركة في السحور تحصل بجهات متعددة، وهي :
Baraka katika daku hupatikana kwa pande nyingi,nazo ni :
اتباع السنة،ومخالفة أهل الكتاب،والتقوي به على العبادة ، والزيادة في النشاط .
Kufuata sunnah,
na kwenda kinyume na watu wa kitabu (mayahudi na manaswara),
na kujipa nguvu kwa hiyo (daku) juu ya ibada,
na kuzidisha uchangamfu (kwa mfungaji).
📚 الفتح (٤/١٤٠)
[ Al-fat’hu (4/140) ]
Na maana ya Allah na malaika kumswalia mja tumeeleza katika makala zilizotangulia kwa kunukuu kutoka kwa wanachuoni nayo ni:
Allah kuwaswalia waja wake ni kuwasifu yaani huwataja kwa sifa zao nzuri huko mbinguni kwa malaika waliokurubishwa yaani walio Karibu na Allah , na Malaika kuwaswalia waja ni kumuomba Allah awasifu na kuwataja kwa sifa zao nzuri huko mbinguni kwa Malaika waliokurubishwa yaani waliokuwa karibu kama vile Malaika walioibeba Arshi ya Allah .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Muharram (Mfungo nne) 1, 1443H ≈ August 9, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Nitumie mawaiza kwenye emal yangu