إلى كل من يسعى لتقريب بين السلفيين والرافضة
KWA KILA MWENYE KWENDA MBIO KWA AJILI YA KUWAWEKA KARIBU BAINA YA MASALAFI NA MASHIA .
Amesema shekh mkubwa wa kishia Afrika ya Mashariki Abdillahi Nassir: Ni matumaini yetu kwamba,baada ya kukisoma kitabu hiki,itakudhihirikia kwamba hakuna hitilafu kubwa hivyo baina ya msimamo wa sunni juu ya hadithi na ule wa ndugu zao shia, hata iwazuie wao kukaribiana na kuelewana..”
📚 Angalia kitabu chake “SHIA NA HADITH majibu na maelezo,ukurasa wa 1.
Na anasema Ja’afar Ammar Mwazoa katika kitabu chake alichokitunga kwa ajili ya kumtusi sheikh Qasim Mafuta-Allah amuhifadhi-:
“…ili kufikia malengo ya kuanzishwa Uwahabi ya kuingiza mifarakano na uadui baina ya safu za waislamu”
📚 Angalia kitabu chake “SHIMO REFU ALILOTUMBUKIA IBN MAFUTA,ukurasa 10
NENO LANGU MWANDISHI:✍🏾
Muislamu tambua kuwa hii ndiyo dini ya kishia hutumia uwongo na hadaa ili kuwanasa waislamu wasiojitambua!
Hivi ni kweli hakuna tofauti kubwa baina ya Mashia na watu wa sunna ?
Tizama itikadi yao Hawa Mashia kwa swahaba mtukufu Omar (Allah amridhie) kwa kweli naona haya kunukuu maneno haya ya Mashia ambayo ni matusi makubwa juu ya swahaba huyu mtukufu lakini kwa sababu ya kubainisha uovu huu nitanukuu:
يزعم الشيعة أن عمر -رضي الله عنه- كان مصابا بداء في دبره لا يهدأ إلا بماء الرجال
Wanadai Mashia kuwa Ummar (Allah amridhie) alikuwa amepatwa na ugonjwa katika utupu wake wa nyuma (ulikuwa) hautulii isipokuwa kwa maji ya wanaume
📚 Rejea:-⇣
الأنوار النعمانية للجزائري ٦٣/١
Al-anuwaaru nnu’maaniy 1/63, cha Al-jazaairiy ]
وقال العياشي -الشيعي- أن من تسمى ب(أمير المؤمنين فهو ممن يؤتى في دبره.
Na amesema Al-‘ayyashiy -Mshia-kwa yule aliyekuwa akiitwa Amir wa waumini (Ummar) basi huyo ni katika wale waliokuwa wakiingiliwa kinyume cha maumbile
📚 Rejea:-⇣
نقله عنه الجزائري في الأنوار النعمانية١٦٣/١
[ Ameyanukuu Al-jazaairiy katika Al-anuwaar nnu’maaniyyah 1/163] .
Hawa ndio mashia na hizi ni miongoni mwa itikadi zao na anapotokea MTU akawaweka wazi na kubainisha itikadi zao za kikafiri humpa jina baya kama Wahabiyah na mengineo ili watu wasimsikilize!
Haya jamani kuna umoja hapa ? na la ajabu zaidi Mashia wanamsingizia Ummar-Allah amridhie-uwongo huu hali ya kuwa wanajua kuwa Aliy bin Abii Twaalib-Allah amridhie- alimwozesha mmoja ya binti Yake Ummar na hili ni maarufu katika vitabu vyao!.
Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde Assha’afiy .
Imeandaliwa na: fawaidusalafiyatz.net
Tovuti:
www.fawaidusalafiyatz.net
🗓️ Toleo la kwanza : Swafar/Mfungo tano:22,1439H sawa na tar.11/11/2017M ,toleo la pili: Mfungo nne 6, 1443H ≈ August 14, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Telegram:
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•