MAKUMI MATATU KWA WEMA WALIOPITA .

(MASIKU) KUMI YA MWANZO YA MWEZI WA MUHARRAM/ MFUNGO NNE KWA WEMA WALIOPITA

قال أبو عثمان النهدي -رحمه الله-:

Amesema Abuu ‘Uthmaan Annahdiy-Allah amrahamu -:

كانوا يعظمون ثلاث عشرات:
العشر الأخير من رمضان،
والعشر الأول من ذي الخجة,
والعشر الأول من المحرم.

Walikuwa wakiyatukuza makumi matatu :

(Masiku) kumi ya mwisho ya Ramadhani,

na kumi la mwanzo la Dhul-hijja /mfungo tatu .

Na kumi la mwanzo la Muharram/mfungo nne.

📚 لطائف المعارف (ص ٣٩)

[ Latwaaifu l-ma’arif, (ukurasa wa 39) ]

Faida ya mfasiri: 🎤

Walikuwa wakiyatukuza makumi haya kwa kufanya yale ambayo sheria imeelekeza yafanywe katika makumi hayo ,katika mwezi huu wa Mfungo nne hakuna ibada maalumu iliyothibiti zaidi ya ubora wa kufunga katika mwezi huu na haswa siku ya kumi (A’ashuraa) ,na vizuri kufunga na siku ya tisa (9) , na kama kumetokea mkanganyiko katika mwezi muandamo ni bora kufunga siku tatu yaani siku ya : 9, na ya 10 na 11 ,ili apate uhakika kuwa ameipata funga ya Ashuraa , ama kulia na kujipigapiga na kufurahi kwa kupika vyakula vizuri katika siku ya Ashuraa huu ni uzushi wa Mashia na maadui wa watu wa nyumbani kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie.

Faida :

Huyu Abuu ‘Uthman Annahdiy -Allah amrahamu -alidiriki zama za ujaahiliyah na alisilimu katika zama za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-,lakini hakumuona Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-, na amepokea hadith kutoka kwa Maswahaba kadhaa, na anahesabiwa katika watu walioishi umri mrefu sana ,kwasababu aliishi miaka mia moja na thelathini (130).

Muandishi: Ismail Seiph Mbonde .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la kwanza: 11,2018M ,Toleo la pili: Dhul-Qaadah 30, 1442H ≈ Jul 10, 2021M.Toleo la tatu: Mfungo nne 7,1443H, sawa na tar:14 August 2021M .

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

   •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *