TUJIKUMBUSHE KATIKA KUWAFAHAMU MASHIA (NO.9)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

​عقيدة الشيعة في أئمتهم​

ITIKADI YA MASHIA KWA MAIMAMU WAO:-

وقد عقد صاحب كتاب الكافي بابا بعنوان:

NA BILA SHAKA KWENYE KITABU (KINACHOITWA) AL-KAAF UMEWEKWA MLANGO KWA ANUANI (INAYOSEMA):-

( باب أن الأرض كلها للإمام )

MALANGO (HUU UNASEMA) KUWA ARDHI (DUNIA) YOTE NI MILIKI YA IMAMU,

, ومما جاء فيه عن أبي بصير عن أبي عبد الله – عليه السلام- قال :

NA MIONGONI MWA YALE YALIYOKUJA KATIKA MLANGO HUO:-

KUTOKA KWA ABUU BASWIIR KUTOKA KWA ABUU ABDILLAH AMANI IWE JUU YAKE AMESEMA:-​

{ أما علمت أن الدنيا والآخرة للإمام يضعها كيف يشاء, و يدفعها إلى من بشاء, جائز له ذلك من الله.}

“(HIVI HUJUI KUWA DUNIA NA AKHERA (ZOTE) NI MILKI YA IMAMU, HUIWEKA PALE ANAPOTAKA NA HUMPA ANAYEMTAKA (NA HIYO) NI ZAWADI KWAKE KUTOKA KWA ALLAH)”​

📚 ​ REJEA:-⇊​

​أصول الكافي (409/1
​[ Usuulul-kaaf:1/409 ]

UFAFANUZI NA MAELEZO KUTOKA KWA MWANDISHI -ALLAH AMUHIFADHI-

yaani mashia wamewapa maimamu wao daraja na nafasi ya Allah kwa sababu Allah ndiye mwenye kumiliki mbingu na ardhi kama alivyosema :

لِّلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ

البقرة ٢٨٤

“Ni miliki ya Allah (vyote) vilivyomo mbinguni na ardhini”

Albaqara:284 .

lakini mashia wanaitakidi na kusema kuwa mbingu na ardhi ni miliki ya maimamu wao kumi na mbili (12) ! , ndiyo maana utawaona wakiwaomba na kutaja majina yao katika shida mbalimbali!,
na minasaba mbalimbali kama vile wanavyofanya katika siku ya ‘Aashuraa wakijipigapiga miili yao na kujijeruhi na huku wakisema: YAA HUSAIN! YAA HUSAIN! YAA HUSAIN! na maana yake ni ewe Husain! ewe Husain! ewe Huseni! yaani ni sawa unapomtaja Allah katika shida mbalimbali ukasema:YA ALLAH! ewe Allah!

enyi waislamu zindukeni na mujiepushe na dini hii ya kishia

Na pia ​Nimeweka anuani hii (ya waislamu wa kigogo na wengineo) kwa sababu sehemu za Kigogo kwa hapa Dar es salaam ni katika sehemu ambazo zimeathirika sana na Ushia na sehemu nyinginezo huu ni ukumbusho kwao.

wanawake wengi maskini wamenaswa na Mashia wakiwemo vijana na wasichana kwa kurubuniwa na kiasi cha pesa na kudhihirishiwa kuwa Mashia ni watu wema sana na wanaojali shida za watu!.

Maskini hawafahamu hawa kuwa Ushia ni dini nyingine kabisa ambayo lau wangeujua uislamu sahihi na lau wangesomewa yale yaliyomo katika vitabu vyao Mashia basi wangestaajabu na wangejua kuwa wamechanganyiwa sumu katika sukari,

lakini maneno haya humnufaisha yule aliyeukunjua moyo wake kwa kuikubali haki,ama yule mwenye kuendekeza matamanio ya nafsi yake na njaa huyu hatonufaika chochote na maneno haya ni sawa na kutwanga maji katika kinu!!​.

Tunamuomba Allah salama .

Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde Assha’afiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net

🗓️ Toleo la kwanza:Swafar/Mfungo tano 20,1439H sawa na tar. 9/11/2017M.Toleo la pili: Muharram /Mfungo nne 9, 1443H ≈ August17, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *