MAWAIDHA KWA WANAWAKE .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

📩 مَوْعِظَـــــةٌ لِلنِّسَـــــاءِ

MAWAIDHA KWA WANAWAKE .

🔻 قَــالَ الشّــيخ ﻋﺒـﺪُ ﺍﻟﺮﺯﺍﻕ ﺍﻟﺒﺪﺭ حفظه الله:

Amesema sheikh Abdul-Rrazaaq Al-badr- Allah amuhifadhi- :

《 ﺇﻥ ﺍﻟﻤﺮﺃﺓ إﻥ ﻋﺎﺷﺖ ﻣﻊ آﺩﺍﺏ ﺍﻻ‌ﺳﻼ‌ﻡ ﻋﺎﺷﺖ ﺣﻴﺎﺓ ﻛﺮﻳﻤﺔ ﻓﺎﺿﻠﺔ ﻓﻲ ﻧﻔﺴﻬﺎ ﺧﺎﺻﺔ ﻭﻓﻲ ﻣﺠﺘﻤﻌﻬﺎ ﺣﻴﺎﺓ ﺍﻟﻜﺮﻣﺎﺀ ﻭﻋﻴﺶ ﺍلأﻓﺎﺿﻞ ﺍﻟﻨﺒﻼ‌ﺀ .

Hakika mwanamke kama ataishi kwa kushikamana na adabu za uislamu ataishi maisha mazuri, (maisha) bora yeye mwenyewe katika nafsi yake na jamii yake (maisha) ya watu wema na maisha ya watu bora watukufu .

⇦ ﻭإﻥ فتنت ﻭﻣﻀﺖ ﻣﻊ ﺩﻋﺎﺓ ﺍﻟﻔﺘﻨﺔ ﻭﺩﻋﺎﺓ ﺍﻟﺸﺮ ﻭﺍﻟﻔﺴﺎﺩ ﻫﻠﻜﺖ ﻓﻲ ﻧﻔﺴﻬﺎ ﻭﻛﺎﻧﺖ ﺳﺒﺐ ﻟﻬﻼ‌ﻙ ﻏﻴﺮﻫﺎ .

na kama (mwanamke) atafitinika na akawafuata walinganiaji wa fitna na walinganiaji wa uovu na ufisadi (basi) ataangamia yeye mwenyewe na atakuwa ni sababu ya kuangamia wengine.

↫ ﻭﻟﺘﺘﺬﻛﺮ أﻧﻬﺎ ﻳﻮﻣًـﺎ ﻣﻦ ﺍﻷ‌ﻳﺎﻡ ﺳﺘﻐﺎﺩﺭ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﺤﻴﺎﺓ، ﻭﺍﻧﻬﺎ ﺑﺠﺴﻤﻬﺎ ﺍﻟﺠﻤﻴﻞ ﻭﻣﺤﺎﺳﻨﻬﺎ ﺍﻟﻔﺘﻨﺔ ﻭﺗﺰﻳﻴﻨﻬﺎ ﻟﻨﻔﺴﻬﺎ ﻭﻓﺘﻨﺘﻬﺎ ﻟﻠﺮﺟﺎﻝ ﺳﻴﺎﺗﻲ ﻋﻠﻴﻬﺎ ﻳﻮﻡ:

na (mwanamke) akumbuke kuwa yeye ipo siku katika masiku atayaacha maisha haya ,na kwamba yeye na umbile lake zuri na uzuri wake wenye fitna , na kujipamba kwake ,na kuwafitinisha kwake wanamume, itamfikia siku (ambayo) :

🔸 تُدرج ﻓﻲ ﺣﻔﺮﺓ
🔸 ﻭيُهال ﻋﻠﻴﻬﺎ ﺍﻟﺘﺮﺍﺏ
🔸 ﻭتأﻛﻠﻬﺎ ﺍﻟﺪﻳﺪﺍﻥ
🔸 ﻭﻳﺬﻫﺐ ﻋﻨﻬﺎ ﺭﻭﻧﻘﻬﺎ ﻭﺟﻤﺎﻟﻬﺎ

Atakusanywa katika shimo .

Na ataporomoshewa juu yake udongo .

Na watamla wadudu.

Na utaondoka urembo wake na uzuri wake .

🔸 ﻭﺗﻜﻮﻥ ﻓﻲ ﺗﻠﻚ ﺍﻟﺤﻔﺮﺓ ﺭﻫﻴﻨﺔ أﻋﻤﺎﻟﻬﺎ، ﻭﻗــﻴﺪ ﻣﺎﻗﺪﻣﺖ ﻓﻲ ﻫﺬﻩ ﺍﻟﺤﻴﺎة

Na atakuwa katika hilo shimo ni mwenye kufungika kwa matendo yake aliyoyafanya , katika yale aliyoyatanguliza katika haya maisha.

ﻓﻘﺪ ﻛﺎﻧﺖ ﻗﺒﻠﻬﺎ ﻧﺴﺎﺀ ﻋﻤﺮﻥ ﺍﻟﻘﺼﻮﺭ ﺛﻢ ﺳﻜﻦ ﺍﻟﻘﺒﻮﺭ!

⏪ ﻓﻠﺘﺘﻖ ﺍﻟﻠﻪ ﺍﻟﻤﺮﺃﺓ ﺍﻟﻤﺴﻠﻤﺔ ﻭلتعد ﻟﻬﺬﺍ ﺍﻟﻴﻮﻡ عدّﺗﻪ ! 》

Na bila shaka (afahamu) kuwa kulikuwepo kabla yake wanawake waliojenga majumba makubwa, kisha wakaishi makaburini !

basi amche Allah mwanamke wa kiislamu na aandae maandalizi kwa ajili ya siku hii!

📚[(ﻣﻮﻋﻈــﺔ ﺍﻟﻨﺴـﺎﺀ ( ٣٩).

Maelezo ya mtarjumu:

Kama mwanamke anataka utukufu na heshima basi ashikamane na uislamu wake , na pia mwanamke akiishi maisha ya kushikamana na dini itakuwa ni sababu ya jamii kutengemaa ,na katika sababu za mwanamke kupotea ni kufuata mila na desturi za kimagharibi katika mavazi na mienendo mingine ,mila ambazo zinamtoa kabisa mwanamke katika mafundisho ya dini yake .

Na mwanamke akumbuke kuwa ipo siku ataondoka duniani na ataingia kaburini sehemu ambayo hakuna kitakacho msaidia isipokuwa matendo yake na kaburi linaweza likawa ni bustani katika mabustani ya peponi au shimo katika mashimo ya motoni.

Na vile vile afahamu kuwa urembo wake hautomsaidia kama alivyosema mshairi:

جَمَالُ الوَجْهِ مَعْ قُبْحِ النُّفُوسِ

كَقِنْدِيلٍ عَلَى قَبْرِ المَجُوسِ

Uzuri wa uso pamoja na ubaya wa nafsi .

(Mfano wake) ni kama kandili iliyowekwa juu ya kaburi la Mmajusi .

Ufafanuzi wa shairi:

Yule mwenye sura mzuri na moyo wake ni mbaya mfano wake ni kama vile taa iliyowekwa juu ya kaburi la mmajusi ,na majusi ni watu wenye kuabudiwa moto na bila shaka mtu aliyefariki na hali anamshirikisha Allah hata tukichukua taa tukaweka juu ya kaburi lake bila shaka hilo halitomsaidia chochote, kwa hiyo mwanamke afahamu kuwa urembo wake hautomsaidia chochote mbele ya Allah bila ya matendo mema .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 13, 1443H ≈ September 20, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *