Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🔺 قواعد الشك في الصلاة.
KANUNI ZA SHAKA KATIKA SWALA (NO.1)
◾️ قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn uthaimin -Allah amrehemu-:
▪️ واعلم أن الشكَّ لا بُدَّ فيه من معرفة ثلاث قواعد:
Tambua kwamba shaka (katika swala) hakuna budi kujua kanuni nne katika hilo :
⏪ القاعدة الأولى: إذا كان الشكُّ بعد انتهاء الصَّلاة، فلا عِبْرَة به إلا أن يتيقن النقص، أو الزيادة
Kanuni ya kwanza:
Itakapokua shaka (imekuja) baada ya kumalizika swala,basi haizingatiwi hiyo (shaka) isipokua akipata yakini ya kupunguza au kuzidisha.
مثال ذلك:
بعد أن سَلَّمَ شَكَّ هل صَلَّى ثلاثاً أم أربعاً؟ نقول: لا تلتفت لهذا الشكِّ، فلا تسجد للسَّهو، ولا ترجع لصلاتك،
Mfano wa hilo:
baada ya kutoa salam ikaja shaka je ameswali tatu au nne?
tunasema : usiigeukie (usiizingatie) hii shaka,basi usisujudu sijida ya kusahau wala usirudi (tena) kuswali swala yako,
لأن الصلاة تمَّت على وَجْهٍ شرعي، ولم يوجد ما ينقض هذا الوجه الشَّرعي،
kwa sababu swala imetimia kwa sura sahihi ya kisheria , na hakujapatikana kinachovunja sura hii sahihi ya kisheria
فالمصلِّي لما سَلَّمَ لا إشكال عنده أن الصَّلاة تامَّة وبرئت بها الذِّمَّةُ، فورود الشكِّ بعد أن برئت الذِّمَّة لا عِبْرَة به.
basi mwenye kuswali pindi alipotoa salamu (anakuwa)hana tatizo kwamba swala imetimia na dhima imeondoka kwa hiyo (swala),basi kupatikana shaka baada ya kuondoka dhima (deni) hakuzingatiwi.
ومثال ذلك: لو شَكَّ في عدد أشواط الطَّواف بعد أن فرغ من الطَّواف،
Mfano wa hilo (pia):
Lau kama atapata shaka katika idadi ya mizunguko katika kuzunguka (al-ka’abah) baada ya kumaliza kuzunguka,
هل طاف سبعاً أم ستًّا؟ فلا عِبْرَة به، فلا يَلتفت إليه؛
Je amezunguka mara saba au sita? basi haizingatiwa (hii shaka) na wala haigeukiwi .
لأنه فَرَغَ من الطواف على وَجْهٍ شرعي فبرئت به الذِّمَّة، فورود الشَّكِّ بعد براءة الذِّمَّة لا يُلتفت إليه.
Kwa sababu yeye amemaliza kuzunguka (al-ka’abah) kwa sura (sahihi ya) kisheria ,na dhima (deni) limeondoka kwa (kuzunguka) huko, kupatikana shaka baada ya kuondoka deni hakugeukiwi (hakuzingatiwi)
ومثله أيضاً: لو شَكَّ في عدد حصى الجِمَار بعد أن فَرَغَ وانصرف، فلا يَلتفت إليه؛
Na mfano wake vilevile:
lau kama itamjia shaka katika idadi ya vijiwe alivyorusha katika viguzo baada ya kumaliza (kurusha) na kuondoka (hii shaka) haigeukiwi (haizingatiwi)
لأنه بفراغ العبادة برئت الذِّمَّة، فورود الشَّكِّ والذِّمَّة قد برئت لا يُلتفت إليه.
kwa sababu hakika hali ilivyo kwa kumalizaka ibada imeondoka dhima (deni) ,kwa kuja shaka hali ya kua dhima imeondoka haizingatiwi shaka hiyo.
📚 [ الشرح الممتع 2/308 ].
Maelezo ya mpitiaji:
Mtu anapomaliza kuswali kwa usahihi kisha ikamjia shaka basi shaka hiyo hatoizingatia kwa sababu ibada yake imemalizika kwa usahihi ,lakini katika madhehebu (ya kishafii) kama mtu atamaliza swala kisha akawa na shaka katika takbiratul-ihraam /takbira ya kuingilia katika swala au nia basi mtu huyo anawajibika kurudia swala ,kwa maana shaka haidhuru baada ya swala isipokuwa katika takbira ya kuingilia katika swala na katika nia kwa sababu mtu hawezi akaingia katika swala ila kwa viwili hivi .
Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 14, 1443H ≈ September 21, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•