KIPIMO CHA UADILIFU.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

◾️‏قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله :

Amesema sheikh ibn ‘Uthaimin-Allah amrahamu-:

إذا أردت أن تعامل غيرك بمعاملة
فقس ذلك في نفســـــك
فإن أحببت أن تعامل بها
فعـــــامل بها غيــــــــرك

Pindi unapotaka kuamiliana na (mtu) mwingine muamala (wowote) basi upime huo (muamala) katika nafsi yako kama ukipenda wewe ufanyiwe (muamala) huo basi mfanyie muamala huo mwingine.

وإن كرهت أن تعامل بها
فلا تعامل بها غيرك

na kama hupendi kufanyiwa muamala huo basi usimfanyie (mtu) mwingine .

وهذا الميزان من العدل
وهو الذي يوجب محبة الناس
للشخص واحترامهم له.

na hiki kipimo ni katika uadilifu ,na hilo ndilo ambalo huthibitisha mapenzi ya watu kwa mtu na humuheshimu

📚 أحكام القرآن الكريم(٤٠٠/٢)

Maelezo ya mtarjumu:

Kama haupendi kufanyiwa jambo fulani basi na wewe usimfanyie mtu mwingine na huu ndiyo uadilifu ,na pindi mtu atapokuwa na tabia hii basi watu watampenda na kumuheshimu .

Na kuamiliana na watu kama unavyopenda waamiliane na wewe ni katika sababu za kuepushwa na moto na kuingia peponi ,kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:

((فمَن أحَب أن يُزحزَح عن النار ويدخل الجنة، فلتأتِه منيَّتُه وهو يؤمن بالله واليوم الآخر، وليأتِ إلى الناس الذي يحب أن يؤتى إليه))

“Basi yeyote anayependa kuwekwa mbali na moto na kuingizwa peponi, basi kimfike kifo chake na hali anamuamini Allah na siku ya mwisho ,na awafanyie watu vile anavyopenda wamfanyie”

رواه مسلم.

Maana ya hadithi:

Katika mambo ambayo ni sababu ya kuepushwa na moto na kuingizwa peponi ni kuamiliana na watu kama wewe unavyopenda waamiliane na wewe bila shaka maneno haya ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- yanazingatiwa kuwa ni kanuni ya kuamiliana na watu na pia ni sababu ya kuenea tabia njema, na lau watu wangeifanyia kazi hadithi hii basi kungeenea mapenzi baina ya waislamu kwa sababu kusingekuwa na khiana ,uwongo, utapeli,hadaa,usengenyi,umbea,n.k ,kwa hiyo ndugu yangu muislamu kila unapotaka kumfanyia mtu jambo fulani basi lipime katika nafsi yako je wewe unapenda kufanyiwa jambo hilo kama hupendi kufanyiwa basi usimfanyie mtu mwingine .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 18, 1443H ≈ September 25, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *