Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🔴 قــــــاعدة عــــــقدية مـــــهمة.
Kanuni muhimu ya kiitikadi .
▫️”كل من اعتقد في شيء أنه سبب ولم يثبت أنه سبب لا کونا ولا شرعا، فشركه شرك أصغر” .
“Kila mwenye kuwa na itikadi katika kitu kuwa ni sababu (ya jambo fulani) na haikuthibiti kuwa hicho (kitu) ni sababu si kikadari wala kisheria basi ushirikina wake ni ushirikina mdogo “
•لأنه ليس لنا أن نثبت أن هذا سبب إلا إذا كان الله قد جعله سببا كونيا أو شرعيا، فالشرعي : كالقراءة والدعاء ، والكوني : كالأدوية التي جرب نفعها.
Kwa sababu hakika hali ilivyo hatuwezi kuthibitisha kuwa hii (ni) sababu ila ikiwa Allah ameifanya kuwa ni sababu (ima sababu) ya kiulimwengu au ya kisheria , na (sababu) ya kisheria ni : Kama kusoma /quran/nyiradi, na (sababu za) kiulimwengu kama vile dawa ambazo manufaa yake yamejulikana Kwa uzoefu.
📗القول المفيد ص ٣٣٨
Maelezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amrahamu- anataja kanuni muhimu mno ya kujua ushirikina mdogo ambao haumtoi mtu katika uislamu ila ni dhambi mzito mno , na mfano wa kanuni yenyewe ni huu:
Mtu atakuwa amemshirikisha Allah ushirikina mdogo kwa mfano: Pindi anapokifanya kitu fulani kuwa ni sababu ya kuondoa maradhi na hali hicho kitu si katika sababu za kisheri ambazo amezitaja Allah au Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kama kusoma quran (ruqya) ,dua .
Na wala ikawa si katika sababu za kikadari nazo ni sababu za ada yenye kuendelea zinazojulikana kwa uzoefu ,yaani sababu zinazoonekana kama vile inafahamika kuwa kumeza paracetamol ni katika sababu za kutuliza maumivu, au mfano ikawa inafahamika kuwa mzizi wa mti fulani pindi utakapochemshwa na kunywa maji yake ni dawa ya tumbo hii pia ni sababu ya kiada haina ubaya kuitumia.
Ama yule mwenye kuvaa hirizi, au ringi mkononi mwake au akavaa chochote, au akachimbia kitu nyumbani kwake, au akaweka mkaa chini ya mto wake wa kulalia, n.k , mwenye kuyafanya haya na akaitikadi kuwa ni sababu ya kuondolewa maradhi au kukingwa basi atakuwa amemshirikisha Allah ushirikina mdogo na ushirikina mdogo ni dhambi mzito mno pamoja na kuwa haimtoi mtu katika uislamu,
ama mwenye kuyafanya haya na akaitikadi kuwa vitu hivi vinamkinga au vinamuondolea maradhi vyenyewe kama vyenyewe basi huu ni ushirikina mkubwa unaomtoa katika uislamu na kumuingiza katika ushirikina na ukafiri .
Ukiifahamu kanuni hii utafahamu kuwa watu wengi wanamshirikisha Allah kama vile madereva mbalimbali ambao hutundika vitu kwa madai ya kinga mbele ya magari yao ! .
Mfasiri: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 21, 1443H ≈ September 28, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Asante