MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU- AMANI IWE JUU YAKE- (23)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUFU -AMANI IWE JUU YAKE .

Makala namba (23) .

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُاْ الآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّى حِينٍ

Kisha ikawadhihirikia (yule Waziri na watu yake) baada ya kuona alama (za usafi wa Yusufu) ni kuwa wamfunge kwa muda kidogo . (35)

وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانَ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ خَمْرًا وَقَالَ الآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْمِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ

Na wakaingia pamoja naye gerezani vijana wawili .Mmoja wao akasema : (kumwambia Nabii Yusufu): “Hakika nimejiona (katika ndoto) nakamua ulevi”.Na mwingine akasema: “Hakika nimejiona (katika ndoto) nabeba mikate juu ya kichwa changu ambayo ndege wanaila.Tuambie tafsiri yake ; kwa yakini sisi tunakuona wewe ni miongoni mwa watu wema ” (36).

Maelezo ya muandaji:

Kisha yule Waziri na watu wake baada ya kuwadhihirikia usafi wa Yusufu kutokana na hayo anayosingiziwa, wakafikiana wamfunge kwa muda mpaka hizi habari zifichikane na zisahaulike, na Yusufu akaingia gerezani pamoja na vijana wawili miongoni mwa watumishi wa Mfalme na imesemwa kuwa waliingizwa gerezani kwa sababu ya tuhuma waliyotuhumiwa na Mfalme ikawa ndiyo sababu ya kufungwa, lakini Yusufu alifungwa bila ya hatia .

Na hapa tunajifunza kuwa Allah anapokadiria jambo hakuna wa kulizuia ,na Allah -aliyetukuka- alikadiria Yusufu aingie gerezani na vijana hao wawili ili mmoja katika hao vijana awe ndiye sababu ya kutoka Yusufu gerezani ,na kudhihiri jambo lake na kuwa mtu mkubwa na mwenye nafasi katika serikali ya kipindi hicho.

Baada ya kuingia gerezani mmoja wao hao vijana akamwambia Yusufu: Mimi nimeota usingizini kuwa ninakamua zabibu ili kutengeneza mvinyo (pombe) .Na mwingine akamwambia : Mimi nimeota nimebeba kichwani mwangu mikate ,na ndege wanaila! wakamwambia Yusufu awaambie tafsiri ya haya waliyo ota.
Na wakamueleza Yusufu sababu yao ya kumfuata yeye awatafsirie ndoto ni kwa sababu walimuona kuwa ni katika watu wema na Yusufu alikuwa maarufu humo gerezani kwa wema wake na ihsani yake kwa wafungwa na ukweli katika mazungumzo,basi hao vijana wawili wakaona kuwa hii ni alama ya kuwa huyu ni mtu mwema, na tumeona katika aya zilizopita Allah- aliyetukuka alisema pale alipomzungumzia Yusufu-:

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (٢٢)

{Na (Yusuf) alipofikia utu uzima tulimpa hukumu na elimu .Na kama hivi tunawalipa wanaotenda mema .

Pia tunajifundisha kuwa ukarimu ,uaminifu,ukweli ,unyenyekevu,kukithirisha ibada ,haya yote ni sababu ya mtu kupendwa na watu ,na pindi mtu anapokuwa mwema basi Allah hudhihirisha huo wema katika mwonekano wake.

Muandaaji: Ismail Seiph Mbonde.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 22, 1443H ≈ September 29, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

2 Comments

  1. Omary Suleiman

    Mashaallah Allah akulipeni khair

  2. Quality content is the main to attract the users to visit the web page, that’s what this web site is providing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *