VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE.

Makala namba : ( 4) na ya mwisho .

✍ قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله:

Amesema shekh ibn Uthaimin -Allah amrehemu-:

⬅️ القسم الرابع:

Kigawanyo cha nne:

:أن لا تطرأ على باله تلك السيئة من الأصل،

(Ni mtu) kutotokea kabisa katika moyo wake mawazo juu ya (kufanya) huo uovu

كرجل لم تطرأ عليه السرقة، ولم يطرأ عليه الزنا، ولا شرب الخمر،

Kama vile mtu (ambaye) hayajamtokea mawazo ya kuiba ,na wala hayajamtokea mawazo ya kuzini, wala (mawazo) ya kunywa pombe,

فهذا ليس له أجر، وليس عليه وزر، لأنه ليس له نية، لا لفعل السيئة ولا لتركها.

Basi (mtu) huyu hapati thawabu wala dhambi ,kwa sababu hana nia ,si ya kufanya uovu wala ya kuacha (uovu).

  • فهذه أقسام أربعة دلت عليها النصوص. Basi hivi vigawanyo vinne (ndivyo) vilivyojulishwa na dalili.

📚 التعليق على مسلم (مج ١ ص ٣٨٠ – ٣٨١).

Maelezo ya mpitiaji :

Na mfano wa kigawanyo hiki pia alichokitaja sheikh -Allah amrahamu- , ni yule aliyekusudia uovu na akaazimia lakini akaacha kufanya huo uovu si kwa kumuogopa Allah, huyu vile vile hapati dhambi wala thawabu, Mfano:

Yule aliyekusudia kufanya uzinifu na akaazimia juu ya kufanya hilo akafanya jitihada katika hilo kisha baadae akafikiria na akaona kuwa hakuna faida atakayopata katika huo uzinifu bali atatoa pesa zake na muda bila ya faida akaamua kuacha ,basi mtu huyu hapati thawabu wala dhambi.

Au mfano mwingine :
Mtu ambaye amekusudia kusema uwongo katika biashara fulani anayoifanya na akaazimia kufanya hivyo, lakini akafirikia akaona kuwa uwongo utamharibia biashara yake kwa kutoaminiwa na watu ,na huyu pia hapati thawabu wala dhambi kama yule wa mwanzo kwa sababu kaacha hayo madhambi si kwa ajili ya kumuogopa Allah, bali ni kwa ajili ya nafsi yake.

Mpitiaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 13, 1443H ≈ October 24, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *