Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
{فَتَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ}
Basi ametukuka Allah mbora wa waumbaji .
المؤمنون:١٤
قال ابن القيم -رحمه الله-:
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
«اقتضت حكمةُ الربِّ الخالق سبحانه أنْ جَعَل ماء الأذن مرًّا في غاية المَرارة،
Hekima ya Mola mlezi muumba-utakasifu ni wake- imepelekea kuyafanya maji ya sikio (kuwa ni) machungu ukomo wa uchungu,
فلا يجاوزُه الحيوانُ ولا يقطعُه داخلًا إلى باطن الأذن،
na mnyama /mdudu hawezi kulivuka na wala hawezi kupita mpaka ndani ya sikio,
بل إذا وصل إليه أعمَل الحيلةَ في رجوعه.
bali kama atafika (ndani) atafanya hila ya kurudi (nje ya sikio).
•وجَعَل ماء العَين مِلْحًا ليحفظها؛ فإنها شَحْمةٌ قابلةٌ للفساد، فكانت ملوحةُ مائها صيانةً لها وحفظًا.
Na akayafanya maji ya jicho kuwa ni (yenye) chumvi ili ilihifadhi hilo (jicho) ,na bila shaka hilo (jicho) ni mboni inayokubali kuharibika, basi kukawa uchumvi chumvi wa maji yake ni yenye kulilinda hilo (jicho) na kulihifadhi.
•وجَعَل ماء الفم عَذبًا حُلوًا ليُدرِك به طُعومَ الأشياء على ما هي عليه؛
Na akayafanya maji ya kinywani ni mazuri na matamu ili (mwanadamu) aweze kuhisi ladha ya vitu kama vilivyo ,
إذ لو كان على غير هذه الصِّفة لأحالها إلى طبيعته، كما أنّ مَن عَرَض لفمه المرارةُ استمرَّ طعمَ الأشياء التي ليست بمُرَّة»
Kwani lau (hayo mate) yangelikuwa hayana sifa hiyo (ya uzuri/utamu) yangevibadilisha hivyo (vitu/vyakula) vikawa katika asili ya hayo mate,kama vile yule ambaye kinywa chake kimeingiwa na (hali ya) uchungu huisi ladha ya uchungu katika vitu ambavyo si vichungu “
مفتاحدارالسعادة (٥٤٤/٢).
Maelezo ya mtarjumu:
Maneno mazito ya ibn l-Qayyim- Allah amrahamu yanayozungumzia katika hekima za Allah katika uumbaji :
1- Allah kwa hekima yake ameyafanya yale maji maji ya masikio kuwa ni yenye ladha ya uchungu tena yaliyofikia ukomo katika uchungu na katika hekima ya hilo ni kutoweza kupita mdudu akaingia ndani ya sikio na kama ataingia basi atafanya kila hila ili atoke kwa sababu ya ule uchungu wa hayo majimaji ya sikio .
2- Na akayafanya maji maji yanayotoka machoni kuwa ni yenye chumvi chumvi ili yahifadhi macho kutokana na kuharibika kwa sababu hilo jicho ni mboni ambayo huwenda ikaharibika kwa hiyo haya majimaji ya chumvi hulizuia jicho lisiharibike na kuoza kwa sababu maji ya chumvi huzuia vitu kuoza na kuvunda kama yalivyo maji ya bahari .
3- Na akayafanya maji yaliyopo kinywani /mate kuwa ni mazuri na matamu na katika hekima ya hili ili mtu aweze kuipata na kuhisi ladha ya vitu kama vilivyo kwa sababu lau kama maji maji /mate yangekuwa hayana asili ya utamu basi ingekuwa kila mtu anapokula kitu ingekibadilisha na kukipeleka katika asili ya hayo mate mfano wa hilo : Ni kama mtu anapopatwa hali ya kuhisi uchungu katika kinywa chake kila kitu anachokula hukihisi kina uchungu hata kama kitu hicho si kichungu !
Mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 21, 1443H ≈ October 27, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•