Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
قال ابنُ الْجَوْزِيّ – رحمه الله تعالى:
Amesema ibn Al-jauziy – Allah aliyetukuka amrahamu
” من أحب أن لا ينقطع عمله بعد موته فلينشر العلم “
” Mwenye kupenda yasikatike matendo yake baada ya kufa kwake basi aeneze Elimu “
التذكرة (٥٥)
Maelezo ya mtarjumu:
Amesema Allah -aliyetukuka-:
{ إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَٰهُ فِىٓ إِمَامٍۢ مُّبِينٍۢ }
{ Hakika sisi tunawafufua maiti na tunayaandika waliyo yatanguliza na waliyo yaacha (nyuma). Na kila kitu tumekidhibiti katika daftari linalobainisha }
Ufafanuzi:
Allah atawafufua waja siku ya kiama na atawalipa juu ya matendo yao waliyoyafanya ya kheri na ya shari. na matendo ya wanadamu yamegawanyika mara mbili:
1 – Kuna yale wanayoyatenda na yakaishia hapo hapo yaani baada ya kufa athari yake si yenye kuendelea kama vile swala, funga n k.
2 – Kuna matendo ambayo athari yake ni yenye kuendelea hata baada ya kufa sawa sawa yawe ya heri au ya shari ,mfano wa matendo ya heri kama vile: Mtoto mwema au matendo ambayo wameyahuisha wao na watu wakawaiga, kama vile kusambaza elimu na mengineyo mengi ambayo athari yake ni yenye kuenea na kuendelea, ila katika matendo haya elimu ni bora zaidi kama alivyosema sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
العلم أفضل بكثير من المال، حتى لو تصدق بأموال عظيمة طائلة، فالعلم ونشر العلم أفضل.
Elimu (ya kisheria) ni bora zaidi ya mali kwa (mara) nyingi hata kama (muislamu) atatoa sadaka nyingi sana ,basi elimu na kueneza elimu ni bora zaidi .
📚 شرح رياض الصالحين لابن عثيمين رحمه الله (٤٣/٥).
Tanbih:
msingi muhimu ni kuwa na ikhlaswi yaani kufanya kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah .
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la pili: Mfungo saba 3, 1443H ≈ November 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•