KOSA KUBWA KWA BAADHI YA WAGONJWA!

◾️ قــال العلامة صالح_الفوزان حفظه الله :

Amesema mwanachuoni mkubwa Swaleh Al-Fauzan-Allah amuhifadhi-:

ﻭﻫﻨﺎ ﻳﺠﺐ اﻟﺘﻨﺒﻴﻪ ﻋﻠﻰ ﺃﻥ ﻣﺎ ﻳﻔﻌﻠﻪ ﺑﻌﺾ اﻟﻤﺮﺿﻰ ﻭﻣﻦ ﺗﺠﺮى ﻟﻬﻢ ﻋﻤﻠﻴﺎﺕ ﺟﺮاﺣﻴﺔ، ﻓﻴﺘﺮﻛﻮﻥ اﻟﺼﻼﺓ ﺑﺤﺠﺔ ﺃﻧﻬﻢ ﻻ ﻳﻘﺪﺭﻭﻥ ﻋﻠﻰ ﺃﺩاء اﻟﺼﻼﺓ ﺑﺼﻔﺔ ﻛﺎﻣﻠﺔ،

Na hapa ni wajibu kutanabaisha kuwa yale wanayoyafanya baadhi ya wagonjwa, na wale wanaofanyiwa upasuaji, (utawaona) wanaacha kuswali kwa hoja kuwa wao hawawezi kutekeleza swala kwa sifa (yake) iliyokamilika,

ﺃﻭ ﻻ ﻳﻘﺪﺭﻭﻥ ﻋﻠﻰ الوضوء، ﺃﻭ ﻷﻥ ﻣﻼﺑﺴﻬﻢ ﻧﺠﺴﺔ، ﺃﻭ ﻏﻴﺮ ﺫﻟﻚ ﻣﻦ اﻷﻋﺬاﺭ،

au hawawezi kuchukua udhu, au mavazi yao yamenajisika, au nyudhuru nyingine zisizokuwa hizo,

❎ ﻭﻫﺬا ﺧﻄﺄ_ﻛﺒﻴﺮ ؛ ﻷﻥ اﻟﻤﺴﻠﻢ ﻻ ﻳﺠﻮﺯ ﻟﻪ ﺗﺮﻙ اﻟﺼﻼﺓ ﺇﺫا ﻋﺠﺰ ﻋﻦ ﺑﻌﺾ ﺷﺮﻭﻃﻬﺎ ﺃﻭ ﺃﺭﻛﺎﻧﻬﺎ أو ﻭاﺟﺒﺎﺗﻬﺎ، بل ﻳﺼﻠﻴﻬﺎ ﻋﻠﻰ ﺣﺴﺐ ﺣﺎﻟﻪ،

na hili ni kosa kubwa kwa sababu muislamu haruhusiwi kuacha swala pindi atakaposhindwa (kufanya) baadhi ya sharti zake au nguzo zake au wajibu zake bali ataiswali hiyo (swala) kwa kadri ya hali yake

ﻗﺎﻝ اﻟﻠﻪ ﺗﻌﺎﻟﻰ:

  { فَاتَّقُوا اللَّهَ مَا اسْتَطَعْتُم }؛

amesema Allah -aliyetukuka-:

{Basi mcheni Allah (kadri) muwezavyo}

ﻭﺑﻌﺾ اﻟﻤﺮﺿﻰ ﻳﻘﻮﻝ : ﺇﺫا ﺷﻔﻴﺖ قضيت اﻟﺼﻠﻮاﺕ اﻟﺘﻲ ﺗﺮﻛﺘﻬﺎ،
ﻭﻫﺬا ﺟﻬﻞ ﻣﻨﻬﻢ ﺃﻭ ﺗﺴﺎﻫﻞ؛

na baadhi ya wagonjwa husema:

Pindi nitakapopona nitazilipa swala ambazo nimeziacha, na huu ni ujinga utokao kwao au uzembe;

ﻓﺎﻟﺼﻼﺓ تصلى ﻓﻲ ﻭﻗﺘﻬﺎ ﺣﺴﺐ اﻹﻣﻜﺎﻥ، ﻭﻻ ﻳﺠﻮﺯ ﺗﺄﺧﻴﺮﻫﺎ ﻋﻦ ﻭﻗﺘﻬﺎ؛ ﻓﻴﻨﺒﻐﻲ اﻻﻧﺘﺒﺎﻩ ﻟﻬﺬا، ﻭاﻟﺘﻨﺒﻴﻪ ﻋﻠﻴﻪ،

na swala huswaliwa katika wakati wake kadri inavyowezekana na wala haifai kuichelewesha na kuitoa katika wakati wake, ni wajibu kuzinduka kwa hili na kuwazindua (wengine)

يجب ﺃﻥ ﻳﻜﻮﻥ ﻓﻲ اﻟﻤﺴﺘﺸﻔﻴﺎﺕ ﺗﻮﻋﻴﺔ ﺩﻳﻨﻴﺔ،

wajibu kuwepo mahospitalini ufahamu wa dini ,

ﻭﺗﻔﻘﺪ ﻷﺣﻮاﻝ اﻟﻤﺮﺿﻰ ﻣﻦ ﻧﺎﺣﻴﺔ اﻟﺼﻼﺓ ﻭﻏﻴﺮﻫﺎ ﻣﻦ اﻟﻮاﺟﺒﺎﺕ اﻟﺸﺮﻋﻴﺔ اﻟﺘﻲ ﻫﻢ ﺑﺤﺎﺟﺔ ﺇﻟﻰ ﺑﻴﺎﻧﻬﺎ .
na kufuatilia hali za wagonjwa katika upande wa swala na mengineyo katika (yanayo) wajibika kisheria , (mambo) ambayo wao wanahaja ya kubainishiwa.

📘الملخص الفقهي (ص ١١٧).

Maelezo ya mtarjumu:

Muislamu haruhusiwi kupitwa na swala hata kama amekosa maji ya kutawadha na udongo wa kutayammamu ni, lazima aswali hivyo hivyo, na hata kama mwili wake na nguo zake zina najisi na akawa hana maji ya kujitwaharishia basi ataswali hivyo hivyo, kwa maana hii ni ile swala ya yule aliyekosa nyenzo mbili za twahara :

(فاقد الطَّهُوْرَيْنِ)

yaani aliyekosa maji na udongo .

Pamoja na kuwa madhehebu yetu ya kishafii yanasema kuwa hizi swala atakuja kuzilipa kwa sababu ya kuziswali kwake bila ya twahara kulikuwa ni kuheshimu muda kwa maana,haifai mtu kupitwa na muda wa swala bila ya kuswali, ila baadhi ya wanachuoni wa kishafii wamechagua kauli ya kutolipa na hiyo ni kauli ya Al-muzaniy -Allah amrahamu- ambaye ni mwanafunzi wa imamu Shafii -Allah amrahamu- na wengineo.

Kwa kifupi : Haifai muislamu kupitwa na wakati wa swala, bila ya kuswali na ni haramu na ni kosa kubwa,.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 18, 1443H ≈ November 23, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *