HUKUMU YA KUFANYA UPASUAJI (OPERATION) KWA AJILI YA KUSAWAZISHA KILEMA AU KIUNGO CHENYE MUONEKANO MBAYA.

السؤال – ٢٤٧

Swali la – 247

أنا فتاة وأعاني من تشوّه في أنفي, وقد جلب لي بعض المشكلات الاجتماعية, والسخرية من قِبَل البعض‏،

Mimi ni msichana na napata shida kutokana na muonekano mbaya wa pua yangu na kwa hakika (hilo) limeniletea baadhi ya matatizo ya kijamii na kudharauliwa kutoka kwa baadhi (ya watu),

وسمعت أنّ هناك عمليات جراحية تعمل لتحسينه، فما هو الرأي الشرعي في ذلك‏؟‏

Na nimesikia kuna upasuaji (operation) unafanywa ili kuifanya iwe vizuri basi ipi rai ya kisheria katika hilo?

الجواب:

Jawabu: 📚

لا بأس بإجراء العملية الجراحية لإزالة التشويه من الوجه وغيره، لأن هذا من العلاج المباح،

Hakuna ubaya kufanya upasuaji (operation) kwa ajili ya kuondoa muonekano mbaya katika uso na (viungo) vingine kwa sababu hii ni katika tiba ya halali,

والغرض منه إزالة الأذى‏،

Na malengo ya hilo ni kuondoa maudhi,

وقد أمر النبي صلى الله عليه وسلم بالتداوي.  

Na bila shaka Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – ameamrisha kujitibia.

📁 المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان.

[ Al-muntaqaa min fatawaa Sheikh Al-fauzan ]

Maelezo kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi

Hukumu hii inaingia pia kwa yule aliyezaliwa na kiungo kilichozidi kama vile akawa na vidole sita au mkono uliozidi na mfano wa viungo hivyo,

Hukumu ya kukikata kiungo hiki ni halali kwa maana ni ruhusa ikiwa hakutopelekea kuangamia au kupata madhara makubwa zaidi, mfano wa kuangamia ni kuwa kama akikatwa kutapelekea kifo na mfano wa madhara makubwa zaidi kama vile ikiwa atakatwa kutapelekea kupata kilema n.k, katika hali hizi mbili haifai kukikata kwa sababu msingi wa kisheria unasema:

” الضرر لا يزال بضرر مثله أو أشد “

“ Madhara hayaondolewi kwa madhara mfano wake au kwa madhara makubwa zaidi ”

Na sheria imeruhusu hilo la kukata kwa sababu ni katika kuondoa kasoro na hilo halijakatazwa isipokuwa sheria imekataza vile ambavyo ni kubadili maumbile kama vile tattoo na mfano wake kwa sababu huko ni kutafuta uzuri zaidi,

Na vile vile upasuaji wa plastiki (plastic surgery) ambao hufanywa kwa ajili ya kuweka vizuri kiungo katika viungo vya mwili vinavyoonekana au hufanyika moja ya hivyo viungo kikipatwa na kasoro au kuharibika au kikawa na muonekano wa kuchukiza, hukumu ya hili inagawanyika sehemu mbili:

1 – Hali ya dharura na hali hii hutokea ikiwa kumepatikana tatizo hilo kutokana na ajali, au vita au kuungua au mtu akiwa amezaliwa hivyo, kwa hiyo katika hali hii mtu anaruhusiwa kukitengeneza kiungo hicho mfano wake ni kama kuondoa chunusi, au vinundu vinavyodhihiri katika uso na sehemu nyingine hakuna katazo la kuviondoa kwa sababu ni aibu zilizojitokeza,

A2 – Aina ya pili ya upasuaji wa plastik ni ile ya khiyari yaani mtu anaamua tu kama vile kuutengeneza uso kwa kuupaka aina fulani ya kemikali au kabadilisha muonekano wa pua au kutumia homon kwa ajili ya kukuza matiti na mfano wa matendo hayo, kufanya hivi ni haramu na ni katika kubadilisha umbile aliloliumba Allah kama alivyosema Allah alipomuelezea shetani:

{ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّهِ}

{ … Na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo yaumba Allah }

النساء: ١١٩
Annisaa: 119

Na kuna makatazo yaliyothibiti katika hadithi ya kukataza kupiga tattoo au kuchonga meno na kuchonga nyusi au kunyofoa na hii ni dalili kuwa hairuhusiwa kufanywa jambo hili la kubadilisha maumbile kwa ajili ya kujiremba.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la pili : Mfungo saba 20, 1443H ≈ November 25, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *