HUKUMU YA RAMBI RAMBI!

https://t.me/fawaidussalafiyatz

☞ HUKUMU YA RAMBI RAMBI !

السؤال:

Swali: 🎙

كان من عادتنا في شمال نيجيريا عند التعزية في بيت الميت

Imekuwa ni katika ada yetu katika (sehemu za) mashariki ya Naigeria wakati wa kutoa taa’zia katika nyumba ya maiti,

يوجد بعض الناس يدفعون عطية من الأموال لأهل الميت،

Kunapatikana baadhi ya watu wanatoa atia (sehemu) katika mali (kuwapa) wafiwa,

هل يجوز هذا أن يعد المال من تركة الميت ويقسم بين الورثة؟

Je, linaruhusiwa hilo na kuzizingatia mali (hizo) ni katika mali alizoziacha maiti na zigawanywe baina ya warithi?

الجواب:

Jawabu: 📚

الأموال تكون ملكاً لمن وهبت له من الأحياء من أقارب الميت،

Mali zinakuwa ni miliki ya yule aliyepewa katika wale waliokuwa hai miongoni mwa ndugu wa maiti,

أما الميت فلا تصح الهبة له إلا من باب التصدق عنه وإهداء الثواب له،

Ama maiti haifai kupewa isipokuwa katika mlango wa kutoa kumtolea sadaka na kutoa zawadi ya thawabu zimfikie huyo (maiti),

ولكن اعتياد الإهداء إلى أقارب الميت حين العزاء بدعة لا أصل له،

Lakini kujizoesha kutoa zawadi ya (mali, pesa) kwa wafiwa wakati wa kutoa taazi’a ni uzushi hakuna dalili (katika jambo hili),

وإحراج للناس المعزين،

Na (huku) ni kuwapa shida wale wanaotoa taazi’a,

وإن المستحب صنعة الطعام لهم،

Na bila shaka lililosuniwa ni kuwatengenezea chakula,

إلا إذا كان أهل الميت فقراء،

ila wafiwa wakiwa ni mafakiri (masikini),

فإنه يستحب التصدق عليهم مما يسد حاجتهم أو يعينهم عليها.

Basi (muda huo) hakika hali ilivyo inasuniwa (ni sunnah) kuwapa sadaka itakayoziba haja zao Au itakayo wasaidia juu ya (haja hiyo).

📚 اللجنة الدائمة(16/432)

[ Kamati ya kudumu (16/432) ]

Maelezo kutoka kwa mfasiri- Allah amuhifadhi

Kawaida ya kuwapa mchango wafiwa (rambi rambi) au kuweka daftari la kuchangia mazishi huu ni uzushi, kwamaana kudumu na hili ni uzushi, ila kama maiti akiwa hana uwezo kwa maana hakuacha mali ya kuweza kukimu gharama za mazishi na watu wakachangishana ili wapate gharama za mazishi,

au wakajitolea baadhi ya ndugu na marafiki hapa hakuna ubaya, ama kudumu na hali hii hata kama maiti ni mtu mwenye uwezo huu ni uzushi kama ilivyotangulia.

kinachotakiwa ni majirani kuandaa chakula na kuwapelekea wafiwa hii ndiyo sunnah, ama wafiwa wakiwa masikini basi ni sunnah kuwa saidia kwa kuwapa sadaka itayowasaidia katika haja zao hata kama ni pesa.

Mwisho kabisa: kwa hiyo tabia ya kuchangishana rambi rambi kila msiba hata kama maiti ana uwezo huu ni uzushi, tena kuna wale ambao wanamuona yule ambae hajatoa kuwa ni bakhili hali ya kuwa hili katika uislamu halipo, na vile vile hakuna kuweka vikundi vya kuzikana katika uislamu!.

Muislamu akifariki kama anauwezo basi ni mali zake zitatumika kumzika au wakajitolea baadhi ya ndugu au marafiki hakuna ubaya na kama hakuna waliojitolea, basi waislamu watajichanga ili kumzika ndugu yao.

Mwisho nawaambia waislamu wenzangu hivi :

Hii siyo dini ya kuiga na kufuata kawaida za wengine.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 29, 1443H ≈ Dec 4, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *