بسم الله الرحمن الرحيم

رسالتي إلى مسلمي شرق أفريقيا عامة وإلى أهل شمازي خاصة.

UJUMBE WANGU KWA WAISLAMU WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA HASWA KWA WATU WA CHAMAZI.

حُكْمُ صُنعِ أهْلِ المَيِّتِ الطَّعامَ للنَّاسِ
عند المذهب الشافعي،

Hukumu ya wafiwa kuwatengenezea chakula watu katika madhehebu ya Shafii,

المقدمة:
Utangulizi:

Nimeamua kuandika kijimakala hiki kwa sababu ya tukio ambalo limetokea katika msikiti wa Vio huku Chamanzi baada ya kijana mmoja kupanda katika membari ya msikiti huo na kuwatuhumu masalafi tuhuma nyingi za uwongo,

kubwa zaidi ni kudai kuwa masalafi wanawagawa waislamu kwa kuleta mizozo katika mambo ambayo hayafai, kuleta mizozo kama vile swala la wafiwa kupika chakula kwa ajili ya watakao shiriki katika mazishi!!

Na akasema kuwa swala hili hata Ibn Baz -Allah amrahamu ameliruhusu!!.

Na huu ni uwongo au hajui kusoma,au atakuwa ameyafahamu vibaya maneno ya sheikh.

Hakuna maneno hayo kabisaa kuwa Ibn Baazi ameruhusu kipikwe chakula kwa washiriki wa mazishi ama kwa wageni kutoka mbali hilo sawa.

kwa kuwa sisi watu wa Afrika ya Mashariki madhehebu yetu ya katika fiqih ni ya kishafii hebu tuone baadhi ya kauli za baadhi ya wanachuoni wetu katika hili pamoja na kuwa madhehebu manne yote yameafikiana juu ya katazo la jambo hilo.

Na hapo tutajuwa kwamba na wanachuoni wakubwa nao wanawagawa waislamu na kuleta faraka?!

قالَ الهَيتَمِيُّ الشَّافِعِيّ فِي شَرحِ المِنهَاج: 

Amesema Al-haitamiy mshafii katika sherh l-minhaaj:

(وَمَا اُعْتِيدَ مِنْ جَعْلِ أَهْلِ الْمَيِّتِ طَعَامًا لِيَدْعُوا النَّاسَ عَلَيْهِ بِدْعَةٌ مَكْرُوهَةٌ كَإِجَابَتِهِمْ لِذَلِكَ،

Na lile lilozoeleka wafiwa kutengeneza chakula ili wawaitie watu (jambo hilo) ni bida’a (uzushi) unao chukiza kama vile kuwajibu kwao (katika wito) huo (pia ni uzushi),

لِمَا صَحَّ عَنْ جَرِيرٍ كُنَّا نَعُدُّ الِاجْتِمَاعَ إلَى أَهْلِ الْمَيِّتِ وَصُنْعَهُمْ الطَّعَامَ بَعْدَ دَفْنِهِ مِنْ النِّيَاحَةِ)

kwa (maneno) yaliyoswihi kutoka kwa Jariir:

(Tulikuwa tukihesabu kujikusanya kwa mfiwa na kutengeneza (kupika) kwao chakula ni katika kulia kwa kupiga makelele).

Ufafanuzi:

Hukumu ya mtu kulia kwa kupiga makelele na kutaja mema ya maiti pindi anapofiwa ni katika madhambi makubwa , kwa hiyo hili la wafiwa kuandaa chakula kwa wote katika msiba limehesabiwa ni katika kulia kwa kupiga makelele msibani au kulia kama njiwa!.

قال الشَّرواني الشَّافِعِيّ في الحاشية: 

Amesema Assharwaaniy mshafii katika Maelezo mafupi (ya kitabu):

” (قَوْلُهُ بِدْعَةٌ مَكْرُوهَةٌ)

(Kauli yake : bidaa inayochukiza )

عِبَارَةُ شَيْخِنَا بِدْعَةٌ غَيْرُ مُسْتَحَبَّةٍ بَلْ تَحْرُمُ “

Maelezo ya sheikh wetu (yapo hivi) : Ni bidaa (uzushi) si sunnah bali ni haramu “

وقَال الغمروايُّ الشَّافِعيّ في السِّراج الوَهَّاج على مَتنِ المِنهَاج:

Amesema Al-ghamrawaay mshafii katika Assiraaj l-wahhaaj ‘alaa matn l-minhaaj:

( وَأما إصْلَاح أهل الْمَيِّت طَعَاما وَجمع النَّاس عَلَيْهِ فبدعة تعد من النِّيَاحَة )

(Na ama wafiwa kutengeneza chakula na kuwa kusanya watu, basi (jambo hilo) ni uzushi na huhesabiwa ni katika kulia kwa kupiga makelele (msibani) )

Neno langu mwandishi:

Tunamuusia hatibu huyu na mfano wa watu hawa wenye kuzungumza mambo wasiyoyafahamu wasome na waache chuki na tunamwambia kwamba akitaka kuijua suna basi akasome kwa watu wa sunnah,

yaani masalafi, ama ukisoma kwa Masufi (watu wa twariqqa) au kwa watu wasio eleweka, wenye kubadilika kama kinyonga tambua kwamba utabakia ni adui wa sunnah (Allah awaongoze) .

Muandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Ilitumwa: June 8, 2018 M, ikarudiwa :Mfungo nane 19, 1443H ≈ Dec 23, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *