قال تعالى حاكيا عن يوسف-عليه السلام- .
Amesema (Allah) -aliyetukuka- hali akisimulia kuhusu Yusufu- amani iwe juu yake-.
يَٰصَىٰحِبَىِ ٱلسِّجْنِ ءَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ (٣٩)
“Enyi wafungwa wenzangu wawili!Je!Waungu wengi wanaofarikiana ndio bora (kuabudiwa) au Allah Mmoja Mwenye nguvu (juu ya kila kitu ?)”
: مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسْمَآءً سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَٰنٍ ۚ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (٤٠)
“Hamuabudu badala yake (Allah) ila majina (matupu) mliyoyapanga nyinyi wenyewe na baba zenu.Allah hakuteremsha dalili kwa hayo .Haikuwa hukumu ila ni ya Allah; ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa yeye tu .Hiyo ndiyo dini iliyonyooka,lakini watu wengi hawajui.
Maelezo :
Yusufu- amani iwe juu yake- aliwaita kwa jina la “Wafungwa wenzangu” kwa sababu hawa vijana wawili aliingia pamoja nao gerezani, na kitendo cha kuegemezewa ufungwa kinajulisha kuwa hawa walikaa gerezani kwa muda .
Hapa tunaona umuhimu wa tauhidi kwa sababu Yusufu- amani iwe juu yake- hakuwaagulia ndoto kwanza bali aliwacheweleshea mpaka baadae na hilo ni kwa sababu la mwanzo kabisa ambalo Manabii na Mitume huanza nalo ni kuwalingania watu katika tauhid yaani kumuabudia Allah pekee na kujiepusha na ushirikina .
Yusufu -amani iwe juu yake- akawaambia je Waungu wengi wanaofarikiana ndio bora kuabudiwa kwa maana : wanaotofautiana katika sampuli na sifa mbalimbali huyu anatokana na jiwe ,huyu wa miti ,huyu wa chuma ,n.k, je hawa ni bora kuabudiwa au Allah mmoja mwenye nguvu juu ya kila kitu .
Na akawaambia kuwa hivi munavyoviabudia si chochote si lolote isipokuwa ni majina matupu mliyoyabuni na kuyapanga .
Na akawabainishia kuwa hukumu zote ni za Allah tu :
1- Hukumu za kisheria.
2- Hukumu za kiulimwengu .
3-Hukumu za malipo .
Na miongoni mwa hukumu za kisheria ni amri ya kumuabudia Allah pekee .
Ama hukumu za kiulimwengu ni yote yanayotokea katika ulimwengu Allah ndiye anaye kadiria.
Maana ya hukumu za malipo ni Allah kusimamia hukumu za viumbe siku ya kiama.
Na akaeleza kuwa tauhid yaani kumuabudia Allah pekee ndiyo dini iliyonyooka kama vile Allah alivyomuamrisha Mtume wake- swala na salamu za Allah zimfikie- aseme:
” قُلْ إِنَّنِى هَدَىٰنِى رَبِّىٓ إِلَىٰ صِرَٰطٍۢ مُّسْتَقِيمٍۢ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ “
Sema: “Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoza katika njia iliyonyooka, (katika) dini iliyo sawa kabisa ambayo ndiyo dini ya Ibrahimu aliyekuwa mwongofu; wala (kabisa) hakuwa miongoni mwa washirikina.”
الأنعام : ١٦٠
Mwisho akaeleza kuwa watu wengi zaidi hawafahamu utukufu wa dini hii kwa sababu ya ujinga wao, na kutofahamu kwao utukufu wa tauhidi kwa ajili hii hawajaamini.
Mwandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 22, 1443H ≈ Dec 26, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•