Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
HALI YA MWANADAMU PINDI ANAPOWEKWA KABURINI!
Amesema Sheikh Swaalih Fauzaan Al-fuzaan – Allah amuhifadhi
❝ Kwa ajili hii hujaribiwa maiti anapowekwa kaburini kwake, basi humjia Malaika wawili na humketisha, hurudishwa roho yake kwenye mwili wake, wanamketisha na wanamwambia:
Nani Muabudiwa wako?
Ni ipi dini yako?
Ni yupi Nabii (Mtume) wako?
Basi muislamu husema: Muabudiwa wangu ni Allah, na dini yangu ni uislamu na Nabii wangu ni Muhammad – swala na salamu za Allah ziwe juu yake,
Na mnafiki na mwenye shaka atasitasita na kutahayari na atasema: Ahaa! ahaa! sijui niliwasikia watu wakisema kitu basi (na mimi) nikakisema hicho (kitu).
Basi (Malaika) watamwambia: Haukujua na wala haukumfuata (mwenye kujua), basi atapigwa na nyundo ya chuma na atapiga ukelele mkubwa kwa (pigo) hilo, kila kitu kitausikia (ukelele) huo Isipokuwa vizito viwili (yaani) Majini na Wanadamu, basi hakuna kuokoka isipokuwa kwa uislamu duniani na akhera ❞
Kusikiliza sauti ya Sheikh, bonyeza hapa: 👇🏾
https://youtu.be/7GA292PoVyU
Maelezo mwandishi:
Haya ni maswali atakayoulizwa mja kaburini na haya maswali ni ile misingi mitatu ambayo imamu Muhammad bin Abdil-Wahhab – Allah amrahamu – ameitungia kitabu akakiita ” Misingi mitatu “
Na yule atakaye yafahamu masuala haya na akayafanyia kazi basi atapewa taufiki ya kujibu maswali haya kaburini,
Ama yule ambaye hutamka maneno haya bila ya kujua makusudio yake kama vile mwenye kutamka tamko la kumpwekesha Allah, lakini akawa hana yakini na kile anachokitamka au mwenye kutamka kwa kuiga au kwa ada, bila ya kuingia katika moyo wake na wengi watakao shindwa kujibu maswali haya kaburini ni mfano wa watu hawa.
Tanbihi:
Muislamu lazima ayafahamu masuala ya itikadi kwa dalili na ayaamini na kuyaitakidi, na linalowajibika hapa ni kujua dalili ya masuala haya ya itikadi kama haya ya maswali ya kaburini japo mara moja katika umri na akaamini na kuitakidi kile kilichojulishwa na dalili na akidumu na hali hii mpaka kufa kwake basi huyo ni muumini aliyekufa katika imani na wala si sharti kwa mtu awe amehifadhi dalili yake na namna ya kutoa dalili lakini wajibu ni kujua na kuitakidi japo mara moja katika umri wake na kudumu na itikadi hiyo mpaka kifo.
Na pia: Maana ya nani Mola wako Mlezi? kaburini ni:
Nani Muabudiwa wako? kwa maana makusudio hapa ni kuulizwa ni nani uliyekuwa akimuabudia duniani na hili ndilo kusudio la kuletwa Mitume ni kuwalingania watu wampwekeshe Allah katika ibada.
Mzungumzaji: Sheikh Swaaleh Fauzaan Al-fauzaan
Mwandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la pili: Mfungo nane 25, 1443H ≈ Dec 29, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•