Faida kutoka katika usia wa imamu Shafii -Allah amrahamu- kwa mwanafunzi wake Al-muzaniy- Allah amrahamu.

Makala namba : (2)

فقلت: عظني

Basi nikamwambia : (Shafii) nipe mawaidha

فقال لي: اتق الله، ومثِّل الآخرة في قلبك، واجعل الموت نصب عينيك،

Akaniambia: Mche Allah ,na ilete picha ya akhera katika moyo wako ,na kiweke kifo mbele yako ,

ولا تنس موقفك بين يدي الله، وكن من الله على وَجَلٍ،

Na wala usisahau kusimama kwako mbele ya Allah ,na kuwa na hofu na Allah ,

واجتنب محارمه، وأد فرائضه، وكن مع الحق حيث كان

Na jiepushe na yale aliyoyaharamisha na tekeleza faradhi zake, na kuwa na haki popote ilipo,

ولا تستصغرن نعم الله عليك، وإن قَلَتِ، وقابلها بالشكر،

Na wala usizidogoshe neema za Allah juu yako hata kama zikiwa chache na kabiliana nazo kwa kushukuru,

وليكن صمتك تفكرا، وكلامك ذكرا، ونظرك عبرة،

Na kuwe kunyamaza kwako ni kutafakari, na kuzungumza kwako (kuwe) ni uradi na kutezama kwako ni mazingatio ,

واعف عمن ظلمك، وصل من قطعك، وأحسن إلى من أساء إليك،
Na msamehe yule aliyekudhulumu, na muunge yule aliyekukata,na mfanyie wema yule aliyekufanyia ubaya ,

واصبر على النائبات، واستعذ بالله من النار بالتقوى.

Na subiri juu ya majanga /matatizo, na jikinge kwa Allah kutokana na moto kwa kumcha Allah .

تاريخ دمشق لابن عساكر ، ج ٥٣ ص ٤٣١ من الشاملة .

Maelezo ya mwandishi :

Al-muzaniy-Allah amrahamu- alimuomba shekhe wake Imamu Shafii -Allah amrahamu- ampe mawaidha na hapa akampa mawaidha na nasaha zilizokusanya nukta 17 :

1- Kumcha Allah kwa maana : Kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake

2- Kuitilia umuhimu akhera kwa sababu dunia ni mapito na akhera ni mahali pa milele ,kama alivyosema.

{ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ }

Na Akhera ni bora na yenye kubaki .

الأعلى : ١٧

Na kauli yake Allah -aliyekuwa tukuka-:

{ وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَكَ مِنَ الْأُولَى }

Na bila shaka akhera ni bora kwako kuliko dunia.

الضحى ٤ .

3- Kiweke kifo mbele yako na tambua kuwa umauti unaweza kukufika muda wowote kama kulivyosemwa:

الموتُ يأْتِي بَغْتَةً *** والْقبْرُ صُنْدُوقُ الْعملِ

Umauti huja.

ghafla na kaburi ni sanduku la matendo.

4- Kumbuka siku utakayosimamishwa mbele ya Allah- aliyetukuka- baada ya kufufuliwa .

5- Muogope Allah ,na kumuogopa Allah -aliyetukuka- kutakupelekea kujiepusha na yale aliyoyakataza .

6- Jiepushe na yale aliyoyaharamisha Allah, na bila shaka hiyo ndiyo njia ya kufikia daraja la ucha Mungu, na katika hadithi ya usia wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- kwa Abuu Hurairah- Allah amridhie-:

اتَّقِ المَحَارِمَ تَكُنْ أَعْبَدَ النَّاسِ،

Jiepushe na yale yaliyoharamishwa utakuwa ni mtu mwenye kufanya ibada zaidi .

رواه أحمد والترمذي

7- Tekeleza faradhi za Allah kwa maana yale ambayo ni wajibu kwako .

8- Kuwa pamoja na haki popote ilipo kwa maana usiangalie mtu bali angalia haki.

9- Usizidogoshe neema za Allah ,tambua kuwa muda wote upo katika neema zake ,kuona kwako,kusikia kwako ,n.k , kithirisha kumshukuru Allah kwa neema zake .

10- Unaponyamaza kimya bila ya kuzungumza muda huo tumia akili yako kwa kufikiria yale yenye manufaa kwako.

11- Unapozungumza jitahidi ukithirishe kumtaja Allah.

12- Na unapotezama tezama kwa mazingatio mfano : Unapovitezama viumbe vya Allah basi mkumbe muumba wake na umuabudu .

13- Msamehe aliyekudhulumu na bila shaka hili lina athari kubwa katika kumrekebisha huyo dhalimu .

14 – Muunge yule aliyekukata kwa kumtembelea au kumsalimia kwa njia mbalimbali na haswa ndugu zako .

15- Na mfanyie wema yule aliyekufanyia ubaya .

16- Kuwa na subira juu ya majanga na mitihani mbalimbali kwa sababu subira mwisho wake ni mtamu kuliko asali.

17- Jikinge na adhabu za Allah kwa kumuabudu .

Inaendelea – Allah akitaka ..

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 1, 1443H ≈ Jan 4, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *